Kamati ya Michuano ya Mapinduzi Cup 2024, imefanya mabadiliko ya timu mbili zilizopangwa kushiriki mashindano hayo kwa msimu huu kutokana kujitoa kwa timu ya Bandari na URA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup, Mbarouk Othman, amesema kutokana na sababu mbali mbali, timu ya Bandari ya Kenya na URA ya Uganda zimejitoa katika mashindano hayo na nafasi zao zitachukuliwa na JKU ya Unguja na Jamus ya Sudani Kusini.
Kupitia taarifa hiyo, Kamati imelazimika kufanya mabadiliko ya Makundi pamoja na ratiba kwa ujumla na kwa sasa makundi yamepangwa kama ifuatavyo:-
Kundi 'A'
Azam FC, Vitalo'o, Chipukizi na Mlandege
Kundi 'B'
Simba SC, APR, Singida FG na JKU
Kundi 'C'
Yanga SC, Jamhuri, KVZ na Jamus.
Mwenyekiti amesema kwa mwaka huu, Bingwa wa michuano hiyo atazawadiliwa Shilingi Milioni Mia Moja (Milioni 100) na Mshindi wa pili atazawadiwa Shilingi Milioni Themanini (Milioni 80).
Michuano itaanza Disemba 28, 2023 katika Uwanja wa Amaan kwa Unguja na Gombani kwa Pemba.
0 Comments