Header Ads Widget

RUWASA KIGOMA YADHAMIRIA KUONDOA SHIDA YA MAJI KWA WANANCHI

 


 Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Kigoma wamesema kuwa wamejidhatiti kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kwa uhakika kwenye vijiji vyote mkoani Kigoma karibu na makazi wanayoishi watu.

Meneja wa RUWASA mkoa Kigoma,Mhandisi Mathias Mwenda alisema hayo katika mafunzo ya siku nne kwa watendaji waaandishi wa RUWASA kutoka wilaya zote za mkoa Kigoma mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Water Mission kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF).

Mwenda alisema kuwa kwa sasa upatikanaji maji vijijini mkoani Kigoma umefikia asilimia 72  na kwamba kuna miradi 25 ambayo inatekelezwa ikiwa kwenye hatua mbalimbali,  ambapo kukamilika kwa miradi hiyo kutafanya upatikanaji maji vijijini mkoani humo itafikia asilimia 85.


Akizungumza katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya jamii wa Shirika la Water Mission walioandaa mafunzo hayo, Rose Mlela alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kubadilishana uzoefu wa namna ya usanifu na utekelezaji wa miradi kwa kutumia mfumo wa umeme jua na kuifanya miradi hiyo kuwa endelevu na kuweza kuyoa huduma wakati wote.

Mlela alisema kuwa mafunzo hayo yanalengaa pia kupeana uzoefu wa namna wadau wote kushiriki kwa pamoja katika utekelezaji wa miradi na uendeshaji wake ikiwemo kuwafanya wananchi kuiona miradi hiyo kuwa ya kwao hivyo kuilinda, kuitunza na kuchangia gharama za uendeshaji ili waweze kuendelea kupata huduma.


Awali Mkuu wa ofisi ya UNICEF mkoa Kigoma, Justus Ndenzako alisema kuwa mafunzo hayo yanawaweka pamoja na kuwajengea uwezo wahandisi na wasimamizi wa miradi inayotekelezwa ili miradi ikamilike kwa viwango, ianze kutoa huduma lakini pia miradi iweze kudumu kwa muda mrefu na kutimiza lengo la kusogea maji karibu na wananchi na kuondoa kero ya kutafuta maji umbali mrefu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI