Header Ads Widget

BENKI YA AKIBA COMMERCIAL BANK ACB YASHIRIKI MBIO ZA ROMBO MARATHONI

Mamia ya wakazi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani  wameshiriki  katika mbio za Rombo marathon, na ndafu Festival yaliyongozwa na Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati mh. Dotto Biteko Yaliyofanyika  katika viwanja vya msitu wa Rongai wilayani Rombo.

Akizungumza na wakazi wilayani hapo  mara baada ya mbio hizo Biteko amewapongeza wote walioshiriki mashindano hayo pamoja na Mbunge wa Jimbo Hilo Prof, Adolf  Mkenda kwa kuanzisha mbio hizo ambazo zinawaleta watu pamoja na kujifunza.


Amesema serikali itawaunga mkono wadau mbalimbali ambao wamejitolea katika kuendeleza shughuli za kijamii ambazo zinasaidia jamii kupata huduma Muhimu ambazo zinaleta maendeleo kwa Taifa.

Wadau walioshiriki katika mbio hizo ni pamoja na Taasisi za Kifedha ambapo moja ya Taasisi hiyo ni Benki ya Akiba Commercial Bank (ACB) .

Akizungumza katika mbio hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya ACB  bw. Silvesta Arumasi amesema kuwa tukio Hilo ni tukio ambalo linaibua fursa mbalimbali ndani ya wilaya ya Rombo, Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla.


"Napenda kuwapongeza washiriki na waasisi wa mbio hizi kwa ujumla kwa jitihada zote walizofanya kufanikisha jambo hili ambalo litakuza taswira ya Rombo ndani na nje ya Nchi." Alisema

Amesema kuwa Benki ya Akiba ACB inatoa huduma Bora na mifumo ya Kidigitali kwa ajili ya kuleta urahisi na wepesi kwa wateja wake na hivi karibuni imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuanzisha huduma mpya kwa lengo la kukidhi mahitaji ya soko.


"Hii pia imefanyika kwa ajili ya kuunga juhudi za Serikali za kuwepo kwa huduma shirikishi za Kifedha (financial inclusion) hivyo basi kwa mwaka mpya wa 2024 wateja wataendelea kunufaika na fursa mbalimbali ndani ya Benki zitakazochochea ukuaji wa Uchumi ,kuinua viwango vya maisha pamoja na Ustawi wa Jamii"Alisema.

Ameendelea kusema kuwa ushiriki wa michezo  ni njia mojawapo ya ya kujenga mahisiano na jamii pamoja na kutoa hamasa ya kufanya michezo kwa watanzania kwa ajili ya Afya njema ya mwili na Akili.


Sambamba na hayo amesema kuwa  ACB imekuwa ikishiriki katika maswala mbalimbali  ya kijamii kupitia sera ya corporate social responsibility ambayo imejengwa  katika misingi ya kusaidia jamii katika sekta ya Afya, elimu,utunzaji wa  mazingira na mambo mengine.

Afisa Masoko wa Benki hiyo  Anton Kunambi amesema kuwa ushiiki wao wa Rombo Marathon ni sehemu mojawapo ya kufanya mazoezi  ambayo yanaimarisha mwili na Akili pamoja na kuwa na fursa ya kukutana na watu tofauti tofauti.


"Tunalenga zaidi kwenye maswala ya kibiashara kwani asilimia kubwa ya walioshiriki Rombo Marathoni ni wafanyabiashara ,na kwetu sisi kama Benki ya Akiba ambao tunadili na kutoa huduma za Kifedha kwa jamii tunapokutana na wafanyabiashara mbalimbali inakuwa ni fursa kwetu"Alisema  kunambi.

Mbali na hayo amewashauri wajasiriamali pamoja na jamii kwa ujumla kuchukuwa mikopo ambayo itawasaidia kulipa ada na katika kipindi Cha Januari kinachokuja.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI