Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WATIA SHAKA UPOTEVU WA FEDHA ZA SERIKALI KATIKA UKARABATI WA UWANJA WA NDEGE TERMINAL II

 


NA MATUKIO DAIMA APP, ZANZIBAR.

CHAMA cha ACT Wazalendo Zanzibar kimedai kwamba Zaidi ya   dola milioni 30 zinatarajiwa kutumika katika  matengenezo jingo  la abiria la pili la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume bila ya kutangazwa zabuni jambo ambalo ni kinyume na sheria ya zabuni iliyopitishwa na baraza la wawakilishi Zanzibar.


Hayo yameelezwa na mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho Ismail Jussa Ladhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa daraja bovu madukani na kuhudhuriwa na makamu wa kwanza wa rais ambae pia ni makamu mwenyekiti wa chama hicho Othman Masoud.


Aiddha Jussa amesema mradi wa ujenzi wa masoko pia umekabiliwa na ufisadi kutokana na gharama za ujenzi kuendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 69.28 mpaka bilioni 102.



Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama hicho Othman Masoud, amesema licha ya kuwepo watu wanaokasirika, wapinzani wanapokosoa lakini wataendelea kufanya kazi hiyo licha ya kuwemo katika serikali ya umoja wa kitaifa.



Naibu katibu mkuu wa chama hicho Nassor Ahmed Mazrui aliendelea kuwakumbusha vijana umuhimu wa kujitokeza katika zoezi la uwandikishaji ammbalo linaendelea ili kupata haki ya kushiriki uchaguzi mkuu.



Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea na miikutano ya hadhara huku wakitumia mudam wingi kuchambua hali ya ugumu wa maisha uliojitokeza Zanzibar na kulalamikia miradi mingi ya ujenzi inakabiliwa na ufisadi bila ya watu wanaofanya vitendo hivyo kuchukuliwa hatua za kisheria zikiwemo kampuni za ujenzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI