Na,Jusline Marco;Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewataka Viongozi wa serikali za mita,vijiji na kata pamoja na wananchi kushiriki vikao mbalimbali vya vinavyoendeshwa katika halmashauri na mkoa ili kuweza kujua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
Makonda ametoa kauli hiyo April 3 wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili kati ya uongozi wa halmashauri ya Jiji la Arusha na wakandarasi kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Esso - Longdong yenye urefu wa kilometa 1.8 kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Ukumbi wa kisasa wa mikutano wa Halmashauri Jiji la Arusha.
Hafla hiyo iliyofanyika katika Kata ya Ungalimited, Makonda amewataka wakandarasi hao kutekeleza miradi hiyo kwa viwango vilivyokubaliwa na kumaliza miradi kulingana na mikataba huku akiwasisitiza wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kadri itavyohitajika.
" Mkandarasi ambaye hataendana na kasi ya mradi tutamtoa kwake anapokaa na kumuhamishia kituo cha polisi awe anatokea hapo kuelekea katika eneo lake la kazi kutekeleza mradi". Amesema Makonda.
Mradi huo wa ujenzi wa barabara utatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 3.2 pamoja na ukumbi wa kisasa kwa gharama ya shilingi bilioni 6.2,kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.
Aidha amesema kuwa mkoa wa Arusha bado haujafanikiwa kwenye eneo la barabara hivyo kusainiwa kwa miradi hiyo kutasaidia kuunganisha kata mbili za Sokoni 1 na Unga limited kuwawezesha wananchi kupitia katika miundombinu kwa urahisi.
Awali akisoma taarifa ya Miradi hiyo Mhandisi wa jiji la Arusha Sifa Edward Makula amesema miradi hiyo ina malengo mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa vikao vya ndani vya halmashauri na kama chanzo cha mapato ya jiji kwa kukodisha kwa wadau mbalimbali watakao hitaji,bapo likikamilika litakuwa na Kumni nne zikiwa na uwezo wa kuchukuwa watu zaidi ya 1400 kwa wakati mmoja huku akieleza lengo la mradi wa barabara.
Sambamba na hayo ametoa wiki mbili kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha na Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuhakikisha nyaraka za ujenzi wa stendi ya kisasa zinakamilika na kusainiwa.
MWISHO.
0 Comments