Header Ads Widget

YAAPA YATOA MKONO WA CHRISTMASS KWA WATOTO WENYE MAHITAJI

 


Mratibu wa Shirika la YAAPA la mjini Kigoma Alex Luoga (katikati mwenye fulana nyekundu) akikabidhi misaada ya chakula  kwa watoto wenye mahitaji wa mjini Kigoma kwa ajili ya sikukuu ya Christmass.

(Picha na Fadhili Abdallah)

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

Shirika la maendeleo ya vijana linalopambana na maambukizi ya HIV (YAAPA) limetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa Watoto wenye mahitai wasio na uwezo wanaosomeshwa na shirika hilo katika masomo ya awali (chekechea) ili kuwafanya Watoto hao kuungana na Watoto wenzao kusherehekea siku kuu ya Christmass.

 


Mratibu wa shirika hilo,Alex Luoga amekabidhi misaada hiyo kwa Watoto hao ikiwa ni kuendana na mpango wa shirika hilo kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu na stadi za Maisha.

 

Luoga alisema kuwa Watoto waliopata misaada hiyo wanatokana na Watoto kutoka familia zisizo na uwezo ambao wanahudhuria masomo ya awali kwenye kituo cha shirika hilo sambamba na Watoto wanaoishi kuzunguka kituo hicho ambao wametambuliwa na mamlaka za serikali za mitaa.

 

Aliitaja zawadi zilizotolewa kwa Watoto hao kuwa ni pamoja na mchele, unga wa ngano, maharage, biskuti na juice na fedha za kufanikisha hilo zinatokana na sehemu ya ada kidogo zinazotolewa na wazazi wa Watoto hao na msaada kutoka Church of Christ True Eternal Light and Love.

 

Akizungumzia misaada hiyo mmoja wa viongozi wa kanisa hilo, Kabwe Litungi alisema kuwa kanisa hilo linashirikiana na shirika hilo katika kusaidia jamii kila uwezo unaporuhusu kufanya hivyo kama ambavyo wamefanikiwa kusaidia misaada hiyo ya chakula kwa Watoto hao.

 

Baadhi ya Watoto hao akiwemo Monica Isack wameshukuru kwa msaada na zawadi hizo kwani zimewafanya kuona kama wao pia wanao watu ambao wanawajali kutokana na  mazingira waliyonayo.

 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI