NA,MATUKIO DAIMA APP,ZANZIBAR.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambae pia Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Masoud Othman amesema kwamba, chama hicho kitaendelea kuwepo Serikalini licha ya kuwepo na changamoto nyingi zinazorejesha nyuma maendeleo.
Makamu mwenyekiti wa Chama hicho ameyasema hayo wakati akihutubia Wananchi katika muendelezo wa mikutano ya hadhara ya Chama hicho ambao mkutano huo umefanyika katika Viwanja vya Daraja Bovu Madukani na kuhudhuriwa na Viongozi na Wananchi mbalimbali.
Amesema kuwa, ACT Wazalendo wataendelea kuwepo katika Serikali ya Umoja wa kitaifa kutokana na Imani yao na mapenzi ya Dhati ya Zanzibar.
Hata hivyo Othman Masoud ameeleza kuwa Chama cha ACT Wazaledo kitaendelea kudumisha Amani na utulivu ulipo ili Zanzibar iendelee kupiga hatua za kimaendeleo.
Mapema, Mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho Ismail Jussa Ladhu adai kuwa kuna matumizi mabaya ya Fedha za Serikali katika ukarabati wa Uwanja wa Ndege Termal II ambapo Mkandarasi amekabidhiwa kazi bila ya kutangazwa kwa zabuni jambo ambalo ni kunyume na sharia za baraza la Wawakilishi.
Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea na miikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali Unguja na Pemba huku wakiwataka Wananchi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura.
0 Comments