Header Ads Widget

PROF MKENDA : VYUO WANDAENI VIJANA WAWE NA UJUZI KUSHIRIKI SOKO LA AJIRA

 

Na Mbaruku Yusuph, Matukio Daima APP. 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ameviagiza vyuo vya elimu ya juu na kati nchini  kuandaa vijana kuwa na ujuzi kwa ajili ya kushiriki katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.


Alisema hayo mwishoni mwa wiki (Agosti 28, 2023) wakati akizindua ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Klkike wanaosoma programu za uhandisi katika sekta ya usafirishaji.


Prof. Mkenda alisema kuwa tatizo la ajira ni changamoto duniani kote, hivyo njia pekee ya kuwasaidia vijana ni kuhakikisha elimu inayotolewa inawaandaa na kuwawezesha kuwa mahiri ili kushiriki na kutafuta ajira popote duniani.



Alisema ni lazima elimu inayotolewa iwe na viwango vya kimataifa na kuwataka viongozi wa taasisi za elimu kuhakikisha zinapeleka wakufunzi wengi zaidi kupata uzoefu, maarifa na stadi katika nchi mbalimbali ili wanaporudi waweze kutoa mafunzo bora kwa vijana.


Aidha, ameongeza kuwa sasa umefika wakati wa vyuo kuanza kutoa zaidi stashahada na kwamba katika kuhakikisha hili linafanikiwa serikali imeanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma stashahada ili kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi na stadi zinazohitajika katika soko la ajira.


Prof Mkenda pia aliweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa majengo matano ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) yanayojengwa kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi na Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariki ( EASTRIP) unaofadhili na Benki ya Dunia (WB) .


Naye Mhandisi Prof. Mganilwa alisema mbali ya kuanzishwa kwa kituo cha Umahiri pia kimeanza kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kike hasa wanaotoka katika mazingira magumu na wale wenye ufaulu wa juu katika masomo kuanzia ngazi ya stashahada hadi Uzamili.


Naye Mmoja wa wanufaika wa ufadhili huo Zawadi Kamote ameishukuru Serikali kupitia chuo hicho kwa kupata ufadhili huo na kwamba ataweka bidii ili kupata matokeo ambayo yatamwezesha kushiriki katika kujenga uchumi wa Taifa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI