Header Ads Widget

DC GEITA ANA CHUKI BINAFSI KWA DED WAKE-JOHN


HATUA ya mkuu wa Wilaya ya Geita Cornel Magembe kutaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Geita Zahara Michuzi kuchunguzwa ni chuki Binafsi kwa Kiongozi huyu wa Serikali ngazi ya Wilaya hiyo.

Kennedy John  akizungumza na matukio Daima Media kwa njia ya simu kutoka Geita  alisema amefuatilia kupitia Vyombo mbali mbali vya Habari taarifa ya DC huyo ila ameona DC kaamua kuonyesha chuki Binafsi kwa Mkurugenzi wake.

"Nachotaka kusema mamlaka ya Uteuzi inatakiwa kuwa makini na huyu DC Cornel Magembe ni mtu anacheza na akili za Watu kwa ajili ya kujifurahisha  na anafanya hivyo kwa malengo binafsi wala si uzalendo kwa Taifa"


Kwani huyu Mkurugenzi insonesha Wazi kuwa  alipata ruhusa kwa kufuata taratibu zote na gharama za safari hiyo hazikulipwa na serikali bali waliomwalika.

Hivyo alisema kuna haja ya  PCCB kufanya kazi ya ziada kumvhunguza vizuri DC kwani insonesha kuna jambo anajificha kupitia mgongo wa Mkurugenzi wake na baada ya kuona safari yake inafika ukingoni kaamua kumchafua Mkurugenzi wake .

Ikumbukwe kuwa huyu DC aliwahi kumchapa makofi DED alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Leo amekuja na vihoja hivi .

Alisema kuna haja ya mamlaka za uteuzi wake kufanya uchunguzi wa kina wa DC huyu kwani Wilaya ya Geita ni Wilaya miongoni mwa Wilaya zenye madini hivyo kuendelea kuwa na DC wa aina hii ni hatari sana .

DC huyu akiwa Ukerewe alikuja na madai ya upotoshaji kuwa zaidi ya shilingi milioni 881 za Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe zilikuwa zimefanyiwa ubadhirifu akiwachafua watu sita akiwemo Mganga Mfawidhi wa Wilaya wa wakati huo (Revocatus Cleophace) huku akitoa siku 14 kwa Mkurugenzi wa Wilaya (wakati huo alikuwa Ester Chaula), Mweka Hazina na Afisa Mapato wa Halmashauri hiyo kurudisha pesa hizo Leo kaibuka na wivu Binafsi dhidi ya Mkurugenzi wa Geita .

 Mkurugenzi wa Geita Zahra Michuzi alisema suala hilo hataweza kulijibia Kwa Sasa na hawezi kubishana na mkuu wake hivyo anavuachia vyombo vya uchunguzi  kuendelea na kazi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI