Header Ads Widget

VIONGOZI WA CCM WAMEAGIZWA KUFANYA ZIARA KATIKA MAENEO YAO KUTATUA KERO ZA WANANCHI-MWENYEKITI CCM MKOA TANGA

 




NA MBARUKU YUSUPH, MATUKIO DAIMA APP TANGA. 


MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Tanga(ccm) Rajabu Abdurahman amewaagiza viongozi wa Chama hicho kwa nafasi zao kufanya ziara katika maeneo yao ili kukijenga Chama hicho na kuimarisha imani kwa wananchi .


Kauli hiyo ametoa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa ambacho ni kikao cha kawaida kilichowakutanisha wajumbe toka Wilaya zote za Mkoa wa Tanga kikiwa na lengo la kukiimarisha chama hicho, kukumbushana baadhi ya mambo na kuhimizana kuhudhuria kwenye vikao mbalimbali vinavyofanywa na Chama.


Aidha alisema kufanyika kwa ziara za mara kwa mara kuna jenga imani hasa kwa viongozi wa chini na wananchi kwa ujumla na ni fursa ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia njia sahihi ya utauzi wake.


"Unajua kupata nafasi ya uwongozi ndani ya chama ni jambo moja na kuitendea haki ni jambo jengine lazima tufanye kazi ya Chama na si vinginevyo"Alisema Abdurahman.


Abdurahman alisema Chama kinakabiliwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na malengo ni kutokupoteza nafasi yoyote kuanzia Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,Vitongoji na Vijiji na lazima wajumbe watambue kuwa hilo ndilo Jeshi la ushindi.


Alisema kila mwana ccm anamatarajio ya kuona Rais anakwenda kupata kura nyingi katika uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa nafasi ya Urais,Wabunge na Madiwani na yasibakie kuwa maneno lazima viongozi wa Chama watoke wakayafanye majukumu hayo kwa vitendo ili kufikia malengo hayo.


"Na ili Rais wetu apate kura nyingi lazima tutoke na tuseme mambo anayoyafanya kwa wananchi wake na kufanya hivi tutakuwa tumevunja nguvu za maadui zetu"Alisema Rajabu.


Hata hivyo aligusia kuhusu mjadala wa uwekezaji wa Bandari ya Dar esa Salaam na Dubai Ports World(DP WORLD) ya Nchini Dubai na kusema wapinzani wanawapotosha Watanzania kuhusiana na mchakato huo ambao unamaslahi kwa Taifa zima tofauti na unavyotafsiriwa na watu mbalimbali.


Alisema Bandari ndio chanzo kikubwa cha pato la Taifa na Serikali imeona ipo haja ya kuiboresha na kutafuta wabia watakaoshirikiana nao ili iwe na tija kwa Taifa na kuondokana na dhana ya ubadhirifu katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya Nchi kwa ujumla.


"Wapo watu wanawapotosha Watanzania juu ya mchakato unaofanywa na Rais wetu juu ya makubalioano na kampuni kubwa ya uwendeshaji wa bandari Duniani ya DPW WORLD na sisi kama chama kazi yetu ni kuwaelimisha wananchi ili Rais wetu aweze kufikia malengo yake"Alisema Rajabu.



Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba alisema Usalama ndani ya Mkoa umeimarishwa ingawa zipo changamoto za biashara za magendo,madawa ya kulevya na uvuvi haramu jambo ambalo Serikali inapambana na nalo.


Kindamba aliyasema hayo wakati akiwakilisha taarifa Serikali katika kikao hicho na alikiri uwepo wa maneno ya upotoshwaji juu ya mchakato wa bandari ya Dar es salaam na jukumu la Chama kumtia moyo Rais na viongozi wenzake ili waendelee na jitihada za makubaliano dhidi ya DP WORLD ya   uwendeshaji wa bandari hiyo.


Hata hivyo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Tanga Rajabu Abdurahman kwa ziara yake katika Wilaya na Halmashauri za Mkoa kwa ukaguzi wake wa miradi ya maendeleo na kutoa maelekezo kwa watendaji wa Serikali.


Alisema ipo haja kwa wana ccm kazi inayofanywa na Mwenyekiti huyo isiishie kwake tu bali ni jukumu la kila kiongozi wa ngazi Wilaya na Halmashauri na hayo ndio makubaliano katika kamati ya Siasa.


Nae Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Tanga Seleman Mzee alisema  Hamashauri Kuu ya Chama hicho katika kikao chake cha kawaida chini ya Mwenyekiti wake Rajabu Abdurahman kimeazimia kwa kauli moja kutoa pongeza na kumshukuru Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ambae ni Mwenyekiti CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anazozifanya kwa Watanzania.


Alisema miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni pamoja na upanuzi mkubwa wa gati la Bandari ya Tanga,kuongeza fedha za maendeleo kwa Mkoa wa Tanga,kuongeza bajeti ya kugharamia sekta ya elimu,kulipia na kuleta ndege ya mizigo ambapo haikuwepo hapo awali.


Alisema mbali na jitahada hizo pia Rais Samia ameimarisha na kudumisha mahusiano baina ya Tanzania na Nchi za jirani sambamba na Mataifa makubwa Duniani,kuimarisha hali ya ulinzi na usalama wa Nchi ili wananchi wawe huru kufanya shughuli zao za kujiongezea kipato.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI