NA AMINA SAIDI,TANGA
Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa kiasi cha sh.8,300,000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya Umoja wa wakulima uhifadhi mazingira Kihuwi Zigi( UWAMAKIZI ),ujenzi wa ofisi ya mtendaji Mbambara na ofisi ya Elimu kata ya kisiwani zilizopo wilaayani Muheza Mkoani Tanga.
Hayo aliyasema Mhifadhi mkuu wa Misitu ,Shamba la miti Longuza Kata ya Amani walayani Muheza Erinema Masalanga wakati akikabidhi msaada wa mbao za kupaulia kwa UWAMAKIZI ikiwa ni moja ya mchango wa maendelea kwa jamii katika kazi za uhifadhi unaofanywa kila mwaka .
Aidha alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wamefanikiwa kutoa vifaa vya ujenzi kwa taasisi mbalimbali ikiwemo ,UWAMAKIZI mbao za kupaulia zenye jumla ya thamani ya sh.3,888,000/=,ofisi ya mtendaji Mbambara mbao za kupaulia zenye thamani ya sh.1,340,000/=ofisi ya idara ya elimu kata ya kisiwani mbao za Kupaulia zenye thamani ya sh.1,800,000/= na ofisi ya CCM-Kata ya Nkumba mifuko ya saruji yenye thamani ya
sh.672,000/=pamoja na gharama za usafirishaji wa vifaa hivyo ambayo ni sh.300,000/=inayofanya jumla kuu ya thamani sh.8,300,000.
Sambamba na hayo Mhifadhi mkuu alitoa witoa kwa wananchi kuzingatia utunzaji wa Mazingira,kuheshimu mipaka ya maeneo ya hifadhi za misitu ikiwa ni pamoja na kuzuia uchimbaji wa madini katika maeneo ya hifadhi hususan hifadhi za mito popote zilipo pia kuwafichua wahalifu na kuchukua stahiki ili kulinda maeneo kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWAMAKIZI Twaha Mbarouk aliwashukuru na kuwapongeza wakala wa huduma za Misitu Tanzania kupitia mhifadhi mkuu ,shamba la Longuza kwa kuwa na utaratibu wa kutoa mchango wa maendeleo kwa jamii zilizopo jirani na hifadhi .
Naye Mkuu wa wilaya Muheza Juma Irando ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo ya ugawaji wa vifaa vya ujenzi alitoa wito kwa wananchi na taifa kwa ujumla kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake katika kuhakikisha rasilimali za misitu na vyanzo vya Maji zinalindwa ili kunusuru mabadiliko ya tabia ya nchi na madhara yake.
0 Comments