Header Ads Widget

CHONGOLO AVUTIWA NA KASI YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA IRINGA



Katibu Mkuu wa chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameeleza kuvutiwa na kasi ya ujenzi  wa Uwanja wa Ndege Iringa na kuagiza ujenzi huo ukamilike Mwezi Oktoba mwaka huu.


Akikagua ujenzi wa Uwanja huo Leo Chongolo alisema kuwa kasi ya ujenzi huo ni nzuri na kuwa mkandarasi wa ujenzi huo ameonesha tofauti kubwa na wakandarasi wa miradi mingine ambao Serikali ikiwacheleweshea fedha nao husimama na kazi .


"Kweli mkandarasi huyu ni wa kipekee na anafanya kazi Kwa Moyo Sana nikuombe uendelee na Moyo huo wa kujituma " 


Hata hivyo Chongolo ametaka ujenzi wa Uwanja huo uende sanjari na utangazaji wa fursa za kitalii zilizopo mikoa ya nyanda za juu kusini vikiwemo vivutio vya utalii.


Awali mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Dkt Jesca Msambatavangu na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati mbali ya kuipongeza Serikali Kwa ujenzi huo wa Uwanja wa Ndege pia walisema kukamilika Kwa Uwanja huo kitafungua fursa za Kiuchumi ndani ya mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani .


Katibu Mkuu Leo anahitimisha ziara yake ya siku sita Katika mkoa wa Iringa Kwa kutembelea majimbo yote ya uchaguzi na mchana wa Leo atafanya mkutano wa Hadhara viwanja vya mwembetogwa mjini Iringa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI