Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, 82, amegundulika kuwa na saratani ya tezi dume ambayo imesambaa hadi kwenye mifupa yake, taarifa kutoka ofisi yake ilisema Jumapili.
Biden, ambaye aliondoka madarakani Januari, alibaini Ijumaa baada ya kuonana na daktari wiki iliyopita kutokana na dalili zilizojionesha katika njia ya mkojo.
Saratani ni aina kali zaidi ya ugonjwa ambao umeainishwa kama "kiwango cha juu" na seli za saratani zinaweza kuenea haraka, kulingana na Shirika la Cancer Research UK.
Biden na familia yake wanasemekana wanatathimini aina ya matibabu. Ofisi yake iliongeza kuwa saratani hiyo haiathiriwi na homoni, kumaanisha kuwa inaweza kudhibitiwa.
Katika taarifa ya Jumapili, ofisi ya Biden ilisema: "Siku ya Ijumaa, aligunduliwa na saratani ya kibofu, yenye alama ya Gleason ya 9 ( Daraja la 5) na metastasis kwenye mfupa.
Rais Donald Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba yeye na Mama wa Rais Melania Trump "wanasikitika kusikia kuhusu kilichobainika hivi karibuni wakati wa wa uchunguzi wa Joe Biden."
"Tunatuma salamu zetu za heri kwa Jill na familia," alisema. "Tunamtakia Joe ahueni ya haraka na yenye mafanikio."
Makamu wa Rais wa zamani Kamala Harris, ambaye alihudumu chini ya Biden, aliandika kwenye X kwamba yeye na mumewe Doug Emhoff wanaiweka familia ya Biden katika maombi yao.
MWISHO.
0 Comments