NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Taasisi ya sekta binafsa Tanzania(TPSF) imefanya mazungumzo ya kujadili namna ya kupambana na usafirishaji haramu wa wanyapori katika maeneo ya mipakani na wadau wa sekta ya umma na binafsi ikiwemo wizara ya maliasili na utalii,Ardhi,kilimo, mifugo na uvuvi, wawekezaji wa mabenki,utalii,uchukuzi na wenye viwanda.
Sambamba na hayo pia walijadili mikakati ya kukuza ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kukuza uwekezaji na ushirikiano.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPSF Raphael Maganga wakati wa mkutano huo alisema anaishukuru USAID Tuhifadhi Maliasili kwa kuuendelea kuwauunga mkono ambapo watajadili njia za kupambana na usafirishaji haramu wa wanyapori, kushughulikia migogoro kati ya wanyamapori na binadamu pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Maganga aliwahimiza washiriki mapendekezo ya kuboresha kwani mradi huo unalenga kujenga uelewa kwa sekta binafsi juu ya umuhimi wa njia katika uhifadhi wa bioanuwai kwa maendeleo ya taifa ambapo wanatarajia kutoka na maazimio ambayo yataendeleza zaidi juhudi zao za pamoja katika kukuza uwekezaji endelevu, kulinda bayoanuai pamoja kupambana na usafirishaji haramu wa wanyamapori katika taifa na kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
“Ni jukumu la sekta zote binafsi kuhakikisha kwamba makampuni yao yanawianisha sera zao ili kuhifadhi mazingira sio tu kwa kizazi cha sasa bali pia kwa siku zijazo” Alisema Maganga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Maurus Msuha alipongeza ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani katika kukuza uhifadhi na maeneo ya mawasiliano nchini Tanzania pamoja na kuipongeza TPSF kwa kuandaa mazungumzo kwa wakati yenye lengo la kukuza ushirikiano na mashirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi katika kukuza uwekezaji endelevu na kupambana na biashara haramu ya wanyamapori.
Dkt Msuha alisema mdahalo huo ni mahususi na ya kisekta katika kukuza minyororo mbalimbali ya thamani ambapo alieleza kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi kwa kuhakikisha kunakuwepo na mazingira bora ya biashara na uwekezaji.
Naye Kiongozi wa Timu ya Usimamizi wa Mazingira na Maliasili kutoka USAID Tanzania Nathan Sage, alifafanua kuwa kuwa serikali ya Marekani imekuwa na ushirikiano wa uhifadhi wa zaidi ya miaka 60 na Tanzania ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, USAID imewekeza zaidi ya dola milioni 100 katika uhifadhi.
Mkuu wa mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasii Thadeus Binamungu alibainisha kuwa mradi unalenga kukabiliana na tishio kwa bioanuwai ya Tanzania ambapo wanatarajia Kujenga uwezo wa kitaasisi kwa wadau wa umma na binafsi, Kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uhifadhi wa bayoanuai na usimamizi wa maliasili na Kuboresha sera.
Hata hivyo washiriki waliwasilisha mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja kuwepokwa haja ya juhudi za pamoja kati ya sekta ya umma na binafsi katika kushughulikia migogoro kati ya binadamu na wanyamapori, kupambana na usafirishaji haramu wa wanyamapori, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uwekezaji na ushirikiano endelevu, kuboresha uhifadhi katika maeneo ya mipakani ili kuvutia uwekezaji endelevu, kuunganisha maisha na uhifadhi pamoja na kuwa na mpango kushughulikia matumizi ya ardhi na changamoto zingine za uhifadhi.
0 Comments