Na,Jusline Marco ;Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda amesema Serikali ya awamu ya sita imejipanga kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa ngazi zote.
Mhe.Kaganda wakati wa ziara yake ya kukagua utekezaji wa miradi ya BOOST katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo katika sekta ya elimu msingi,serikali imetoa shilingi milioni 961.5 fedha za BOOST kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu katika shule za msingi ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora katika mazingira rafiki.
Aidha Mhe.Kaganda ameelekeza miradi inayotekelezwa kuwa na viwango na ubora unaotakiwa sambamba na kutekelezwa kwa wakati .
Awali akizungumza katika ziara hiyo Diwani wa Kata ya Majengo Mhe.Bernard Kivondo amemshukuru Rais.Dkt.Samia kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo katika shule ya Msingi Kaloleni kwa awamu ambapo Serikali kupitia TASAF ilitoa milioni 74 za ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa na ofisi.
Aidha Mhe.Kivondo ameongeza kuwa serikali pia ilitoa fedha shilingi milioni 12.5 za ukamilishaji wa boma na sasa imetoa shilingi Milioni 106.3 fedha za mradi wa BOOST kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na vyoo .
Nao baadhi ya wananchi wa Kijjiji cha Kaloleni Kata ya Majengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu kwa kutoa fedha shilingi Milioni 106.3 za ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na vyoo vya wanafunzi wa kike matundu manne.
0 Comments