Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Jumla ya timu 14 za waendesha bodaboda katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Buhigwe zimeanza mashindano ya kuwania kitita cha shilingi milioni tatu katika ligi ya bodaboda hao inayoendeshwa na kituo cha Radio cha Main FM cha mjini Kigoma.
Mkurugenzi wa kituo cha radio cha Main FM,Paschal William alisema kuwa katika mashindani hayo yanayofanyika uwanja wa Kawawa Ujiji mjini Kigoma, pamoja na zawadi hizo pia wachezaji wote na mabenchi yao ya ufundi watafaidika na mafunzo ya ujasiliamali, masualaa ya usalama barabarani, nishati safi na masuala ya afya.
William alisema kuwa katika mashindano hayo Mshindi wa kwanza ataondoka na zawadi ya shilingi milioni 1.5, mshindi wa pili Milioni moja na mshindi wa tatu ataondoka na shilingi 500,000 na kwamba mashindano hayo yanalenga kutoa ujumbe kwa jamii kwamba bodaboda ni kazi yaa maana sana kama zilivyo kazi nyingine na siyo ya kudharauliwa.
Katika mchezo wa ufunguzi timu ya Kombaini ya Kijiji cha Mnanila wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imeitoa timu ya Kombaini ya Bangwe kwa kuifunga penati 3-0 baada ya dakika 90 kutoka suluhu ya kufungana bao 1-1.
Paschal William Mkurugenzi wa kituo cha Main FM cha Mjini Kigoma
Kwa upande wake Msemaji wa mashindano hayo, Steven Ndorobo alisema kuwa pamoja na fursa mbalimbali zilizotolewa kwenye mashindano hayo pia wamewaalika viongozi wa timu mbalimbali kuangaalia vipaji vya wachezaji kuweza kusajili wachezaji watakaoona wanawafaa.
Ndorobo alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa yanaendeshwa kwa mtindo wa mtoano na yatakuwa yanafanyika kila mwishoni wa wiki kwa michezo miwili kupigwa kila wiki na kwamba mashindano hayo yataibua vipaji vingi ambavyo vinaweza kupata nafasi ya kuendelezwa.
Mwisho.
0 Comments