MSTAHIKI meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema kuwa wnanchi hasa Machinga wa Iringa wamekuja na mabango ya kumpongeza MNEC Salim Abri Asas Kwa kazi kubwa anayofanya .
Ngwada ameyasema hayo Leo Katika mkutano wa Hadhara wa katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo uliofanyika Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa.
Alisema siku tatu zolizopita CHADEMA walifanya mkutano wao Iringa na kupitia mkutano huo walielekeza mashambulizi Kwa Asas kwanini anasaidia wananchi Iringa .
Hivyo alisema mabango hayo wameshika kama sehemu ya kumtia Moyo Mnec Salim Abri Asas Kwa Moyo wa kujitolea .
Katibu Mkuu Mimi ndio Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa sisi Manispaa ya Iringa hatukuwa na Shilingi Milioni 200 za kujenga mabanda ya Machinga Mlandege ila Asas kachangia .
Ila Iringa ilikuwa haina wodi ya watoto njiti Asas amejenga Katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ,pia wakati wa Corona amesaidia mitungi ya hewa na mambo Mengine mengi amefanya ndio sababu ya wananchi Iringa kuendelea kumkubali na kumtia Moyo Asas .
Ngwada alisema yeye kama meya wa Manispaa ya Iringa anamuomba Asas kuendelea kusaidia maendeleo ya Manispaa ya Iringa na asiwasikilize wasiopenda maendeleo .
0 Comments