Header Ads Widget

WAZIRI AWESO ATAKA TAFITI ZIFANYIKE ILI KUONGEZA VISIMA VYA MAJI DODOMA

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


WAZIRI wa Maji Juma Aweso ameagiza utafiti kuendele kufanyika mara kwa mara katika jijini la Dodoma ili kugundua wapi kunamabonde ya maji na kuongeza visima vingi vya maji Dodoma hali itakayopelekea kukabiliana na Changamoto ya maji.


Maagizo hayo ameyatoa leo wakati wakipokea mabomba ya maji katika eneo la mradi Nzuguni Jijini Dodoma ambapo amemuagiza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Duwasa kuhakikisha mradi huo hauna Visingizo vyovyote na kuhakikkisha vifaa vinavyotakiwa kwenye mradi huo vinaagizwa mapema.


Aidha amewata  Mkandarasi wa Mradi waaji Nzuguni kuhakikisha wanatekeleza mradi huo bila kuleta visingizio baada ya Malipo ya awali kufanyika .


"Mradi huu wa Nzuguni ambao siku ya leo tunatandaza mabomba unatakiwa kukamilika ifikapo mwezi wa nane mwaka huu," Amesema Waziri Aweso.



Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Duwasa Mhandisi Aron Joseph akitoa taarifa juu  ya mradi huo amesema mradi umefikia asilimia 37.5 ambapo ni hatua ya ujenzi wa vibanda,mitaro ya kusimika mabomba ya maji .


Mhandisi Aron amesema tayari wamefanya malipo ya awali kwa wakanadarasi wa mradi huo hivyo wanategemea ndani ya miezi sita hadi nane kukamilika kwa mradi huo wa maji.


Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema watahakikisha wanafanya malipo kwa wakandarasi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.


Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji DUWASA Prof Davis Mwamfupe amesema kupitia mradi huo wa maji wananchi wa Nzuguni wamekuwa na Mwamko mkubwa na kuahidi kuwa wataendelea kuwa Bega kwa Bega na DUWASA katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.



Naye Diwani wa kata ya Nzuguni Aloyce Luhega amesema kupitia mradi huo ni historia ya wananchi wa Nzuguni kutokana na eneo hilo tangu uhuru halijawahi kuwa na chanzo cha maji safi na salama .


Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya Nzuguni wamesema uwepo wa mradi huo ni hatua kubwa ya kuwapunguzia adha ya maji ambapo walikuwa wakitumia maji ya visima yasio safi na salama na itawapunguzia umbali wa kufuata huduma ya maji.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI