Header Ads Widget

MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI KUCHUKULIWA HATUA BAADA YA KUTAFUNA HELA ZA SHULE ZA UMEME




Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha vijijini kimesema kitamchukulia hatua Kali Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Costantino Mwakamo kwa tuhuma za kuchukua fedha za kuweka umeme kwenye shule ya msingi Ruvu Minazi mikinda shilingi milioni 2 kwa matumizi binafsi baada ya kumlazimisha Mwalimu Mkuu wa shule hiyo atoe kwenye akaunti ya Shule hiyo ampatie mdogo wake Vicent Mwakamo.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibaha vijijini Mkali Kanusu akiwa ameambatana na Sekretarieti ya CCM Wilaya hiyo baada ya kufika Shule ya msingi Ruvu Minazi mikinda kukagua Mirada ya Maendeleo na kubaini kiasi cha fedha kilichotolewa na Mbunge huyo kwa kazi ya kuweka umeme Shuleni hapo hakiendani na kazi iliyofanyika.


Kanusu amesema gharama ya uwekaji umeme katika chumba hicho cha darasa ni kama shilingi 120,000/- lakini wao wakaandika ni shilingi 1500,000/- na milioni moja na nusu nyingine waliiandika iliweka umeme kwenye nyumba ya Mwalimu Shuleni hapo jambo ambalo sio kweli.


Kanusu amesema Fedha iliyotolewa kutoka mfuko wa jimbo ni shilingi milioni 3 lakini baada ya Sekretarieti hiyo kumhoji Mwalimu Mkuu Bakari Kitenge ikiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalawa na Mtendaji Kata ya Ruvu Bi Pili Mgumba ndipo Mwalimu Mkuu huyo alifunguka kwamba baada ya fedha hizo kuingizwa kwenye akaunti ya Shule alipigiwa simu na Mbunge Mwakamo akimtaka kutoa shilingi milioni 2 na kumkabidhi mdogo wake Vicent Mwakamo na kiasi kinachobaki afanyie kazi iliyokusudiwa.


Alisema anasikitishwa kwa tabia hiyo na kwamba CCM Ina Mashaka na tabia hiyo kuwa inawezekana pia katika Miradi mingine ya Maendeleo Mbunge huyo atakuwa amefanya hivyo hivyo,


Aidha amewataka waliopewa dhamana mbalimbali katika Uongozi kuthamini jitihada anazofanya Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa Wananchi wake kwa kuhakikisha Miradi inatekelezwa katika viwango na ubora uliokusudiwa na bila kudhurumu haki yao.


Nilipata kuongea na Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Mheshimiwa Michael Mwakamo kujibu tuhuma hizo amesema hajui kuhusu hizo hela.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI