Na Shomari BINDA-Matukio Daima
Mchango uliotolewa na mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara kwenye Bajeti ya Wizara ya Elimu kuhusu umuhimu wa masomo ya Sayansi umepokelewa vyema na wananchi.
Wakizungumza na Matukio Daima jana mei 12,2025 wakati wakifatilia michango ya wabunge kwenye bajeti hiyo wamesema kile ambacho kimechangiwa na mbunge Waitara kina umuhimu mkubwa
Mmoja wa wananchi hao aliyekuwa akifatilià eneo la garden manispaa ya Musoma Juma Kitundu amesema katika soko la ajira la sasa wana sayansi wana nafasi kubwa.
Amesema alichokichangia mbunge huyo kina ukweli kuhisu mitaala mipya ya elimu kuzingatia suala la kuwapa uelewa walimu ili wafundishe wanafunzi kwa tija.
Juma amesema masomo ya sayansi yana nafasi kubwa kwa sasa lakini zipo nyenzo za ufundishaji zinazohitajika ambazo zinapaswa kuwepo shuleni zikiwemo maabara.
" Nimekuwa nikimuelewa sana mbunge Waitara kwenye michango yake anapokuwa bungeni na anapochangia masuala mbalimbali.
" Kwenye hili la Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia aliochangia kuhusu umuhimu wa sayansi na masuala ya mitaala mipya ya elimu kwa upande wangu nimemuelewa",amesema
Akitoa mchango wake hapo jana bungeni kwenye Bunge la 12 Mkutano wa 19 mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara moja ya mchango wake ni kutokupuuza masomo ya sayansi na kuyapa umuhimu.
Waitara amesema yapo masuala mengi yanayofanyika kupitia sayansi na kutaka wale wanaosoma masomo hayo kuwapa nafasi ya kusoma na wanaosoma masomo mengine wasome.
Katika masuala ya mitaala mbunge huyo alishauri umuhimu wa lugha ya ufundishaji na kushauri walimu waelimishwe na kuongezewa uelewa wa ufundishaji ili waweze kufundisha wanafunzi kwa tija.
0 Comments