NA MWANDISHI WETU, MTWARA
Wananchi wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma wametakiwa kuweka kipaumbe kupanda miti ya matunda na mbogamboga ikiwemo mipapai nyumbani kwao ili kuweza kuboreshea afya na kuwaongezea kipato.
Akizungumza na watumishi wa halmashauri ya mji Nanyamba na waandishi wa habari waliotembelea taasisi ya utafiti wa kilimo tanznaia TARI kituo cha naliendlee kujifunza Mkurugenzi wa TARI kituo cha Naliendele, Dk. Fortunas Kapinga alisema kuwa kilimo cha mapapai kina tija.
Alisema kuwa endapo mtu akilima Mapapai ambayo ni mbegu bora ana uwezo wa kupata fedha hadi shilingi 100, 000 kwa kila mti Mmoja wa Papai kutokana na mipapai hiyo kuzaa kwa wingi
“sisi huwa tukivuna tunawauzia watumishi wetu kwanza kwaajili ya kuboresha afya zao ili wapate afya njema na chakula ambacho kina uhakika na usalama tunafanya ambapo tunauza kwa shilingi 1,000 tu kwa moja na tunapata pesa ya kutosha kwa mti mmoja”
Nae Katibu Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC), Bryson Mshana safari hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo imewajumuisha na watafiti ili kuona kazi wanzofanya na jinsi wanavyotumia teknolojia kuborehsa kilimo nchini.
Alisema kuwa tumekuwa tukiandika habari nyingi na kuhamasisha jamiii kutumia mbegu bora lakini leot tumekuja wenyewe kupata mafunzo ili kutoa taarifa ambazo na sisi wenyewwe tutakuwa na uelewa nazo.
“Hapa tuko wanahabari zaidi ya 30 tumekuja kujifunza lakini tumevutiwa nah ii bustani ya mbogamboga ambayo ina papai moja lenye uzao ambao ukiweza kupanda nyumbani kwako unaweza kufanya biashara na kukaingiza kipato bila usufumbufu”
“Elimu hii inaweza kuokoa watanzania wwengi ambao wapo tu majumbani wana ardhi lakini wanashindwa kujua watumieje ardhi hiyo kwa manufaa yao”
Naye Rajab Susu ambaye ni mtumishi wa halmashauri ya Mji Nanyamba, akakiri kunufaika na elimu juu ya kilimo cha mbogamboga waliyoipata kutoka kwa wataalamu wa TARI, na kuahidi kwenda kuifanyia kazi hasa kwenye mbegu bora ya zao la papai
“Unajua wengi hatuna elimu tu wakati mwigine tunajua kuwa TARI ni korosho, ufuta na karanga lakini kumbe kuna mbogamboga, Mihogo na mzao mengine ni vema kutembelea na kujifunza zaidi binafsi nitarudi hapa kwaajili ya kujifunza zaidi kwenye hilo papai”
0 Comments