Header Ads Widget

WANANCHI MAKAMBAKO NJOMBE WATAKA KUTATULIWA KWA KERO ZAO

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Serikali imetakiwa kutatua kero za wakazi wa Makambako mkoani Njombe zinazotokana na uzembe wa baadhi ya viongozi wanaotoa ahadi zisizotekelezeka zikiwemo za kupelekwa kwa fedha za maendeleo kwenye baadhi ya miradi bila mafanikio.



Katika mkutano wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Kanda ya Nyasa mjini Makambako chini ya  mwenyekiti wake Mchungaji Peter Msigwa amesema ili kuondokana na fikra mgando za miaka mingi kwa baadhi ya viongozi wa serikali chini ya chama cha mapinduzi ni lazima kufanyika kwa marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo imempa mamlaka makubwa Rais katika kuliongoza taifa.



Awali mwenyekiti wa chadema mkoa wa Njombe Rose Mayemba amesema wananchi wa makambako wamekuwa kwenye adha kubwa ya kukosa maji,huduma za afya,biashara na changamoto za elimu kwa kudanganywa na baadhi ya viongozi wao  hivyo suluhu pekee ni kufanya mabadiliko ya viongozi  wasio na maono.



Kwa upande wake mbunge wa zamani wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi[sugu] amesema chama cha mapinduzi ccm kinapaswa kuondolewa mamlakani kwa kushindwa kuaminika.


Kando ya mkutano huo baadhi ya wananchi wa makambako akiwemo Wisman Nyagawa na Elizabeth Ngimbudzi wamekiri kuwa yale yaliyosemwa na viongozi wa Chadema yana uhalisia mkubwa na ndio kiu yao kwani wamekuwa na kero nyingine za kunyanyaswa na Watoza kodi kwenye ujasiriamali wao,kukosekana kwa maji ya uhakika kwa miaka mingi pamoja na usimamizi duni wa miradi ya maendeleo.


Chadema kanda ya nyasa chini ya mwenyekiti wake Mchungaji Peter Simon Msigwa wanaendelea na mikutano yao katika mkoa wa Njombe  ikiwa na lengo la kukiimarisha chama pamoja na kudai mabadiliko ya katiba mpya.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI