NA MWANDISHI WETU MTWARA,
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amewapongeza BRELA na maofisa biashara katika mafunzo ambayo amesema kuwa yatawasaidia kujiboresha katika utendaji wao wa kazi.
Akitoa neno katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili na Biashara (BRELA), wakishirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Wekezaji na viwanda alisema kuwa wamefanya mafunzo hayo kwa maafisa biashara 100 kutoka mikoa 10 ya Tanzania Bara yaliyofanyika Mkoani Mtwara.
“Mmefanya jambo kubwa kuwakutanisha hawa maafisa biashara ni wapongeza waandaji wa mafunzo ya sheria za biashara mafunzo haya ni fursa kubwa na muhimu kwenu kuijua sheria iwasaidie kazini” Kanali Abbas.
Nae Kaimu Mkuu wa sehemu za leseni za biashara wa Brela, Tawi Godfrey Kilumile, amesema wameandaa mafunzo hayo ya sheria ya leseni za biashara na sheria ya taifa ya usajili na utoaji wa leseni za viwanda.
“Tutatoa mafunzo haya kwa maafisa biashara kwa ajili ya kuwajengea uwezo na uelewa wa sheria na kuimarisha utendaji kazi wao katika kuwasimamia na kuwashauri na kuwaelekeza wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali wanaokuja nchini kuwekeza ama kufanya biashara”
“Tumewakutanisha mikoa 10 hivyo wako 100 ikiwa ni mwendelelezo wa mafunzo ya awali ambayo yalijumuisha maafisa bashara wengi zaiid ili kuimarisha sheria na utendaji kazi. alisema ilumile.
0 Comments