NA MWANDISHI WETU, MTWARA
Wakulima wa vijiji vya Ilala, Mangopachanne na Mbagala Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wamevuna mbegu bora aina tisa za muhogo katika shamba darasa wakishirikiana na watafiti wa zao hilo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI Kituo cha Naliendele.
Akizungumza wakati wa mavuno hayo Abdulahman Ekapu mkazi wa mbagala pachanne mkulima wa zao la muhogo alisema kuwa zao hilo ni tegemezi kwake kwakuwa amekuwa akilima kwaajili ya biashara na chakula nyumbani.
Alisema kuwa elimu hii ya tafiti shirikishi ni elimu bora ambayo serikali imeona inafaa kwkauwa sio tu tunafanya kwa vitendo lakini tunafanya wenyewe kwa maelekezo ya watalaam.
“Unajua utafiti shirikishi umetutoa kwenye kilimo cha zamani kisicho na tija na kutuleta kwenye kilimo cha kisasa chenye tija na imetusaidia kujua mbegu za kisasa na mbegu za asilia utofauti wake”
“Hizi mbegu zina tija unapata mavuno mengi kwa kilimo hiki muhogo tena hauna sumu na pia ni mtamu unafaa ni salama pia kwa afya wakulima” alisema Ekapu
nae afisa kilimo kata ya mangopacha nne Irene Ngowi alisema kuwa kupitia shamba darasa hilo wakulima wamejifunza mambo mengi kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna hali ambayo itawabadilisha na kuwafanya waanze kulima kisasa zaidi.
“wakulima wamejifunza na wameona mbegu gani nzuri zinawafaa kwa chakula na biashara ni vema watafiti wakaweka mikakati ya kutuletea mbegu inayofaa kwa wingi na kwa wakati hata kama ni kwagharama iwe nafuu tununue” alisema Ngowi
kwa upande wake Mtafiti Msaidizi kutoka TARI Naliendele Dwasi Gambo alisema kuwa wakulima wameshirikishwa katika utafiti huo kwa asilimia 100 katika uandaaji wa shamba, palizi, kuvuna kupika na kuonja ili kujua radha na rangi pia.
“Leo tunavuna mbegu kwakujumuisha wakulima katika shamba darasa lenye mbegu aina tisa ili kuwafanya wakulima waweze kutambua na kuzifahamu mbegu zote na kuona ipi ni bora kwao”
0 Comments