Header Ads Widget

CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI KUANZA KUTOA MAFUNZO YA URUBANI


NA MATUKIO DAIMA MEDIA

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Ludovick Nduhiye  ameutaka uongozi wa chuo cha Taifa cha Usafiraji (NIT) kuhakikisha wanatunza na  kuendeleza vifaa kwa ajili ya mafunzo ya Urubani, Wahudumu wa Ndege na Wahandishi wa ndege.


Nduhiye amesema  hayo baada ya kutembelea na kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunua na Serikali katika kufundishia mafunzo ya Marubani na Wahudumu wa ndani ya Ndege.


“Serikali imewekeza fedha nyingi katika kununua vifaa hivyi vya kufundishia marubani hivyo uongozi wa chuo unakiwa kuhakikisha vifaa hivi vinatunzwa ili vitumu kwa muda mrefu” Alisema Nduhiye.

Pamoja na kukagua  na kutembelea vifaa hivyo pia alikagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike na wakiume  majengo ya utawala ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 98 na unatarajiwa kukamilika kwatikati ya mwaka huu.


Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Dkt. Prosper Mgaya amesema kuwa vifaa vyote vya  kufundisha urubani katika chuo  vimekalika na mafunzo hayo yanatarajia kuanza Mwezi sita  mwaka huu Huku.

“ Vifaa vya kufundishia Urubani vimekamilika na tumeshapata idhini kutoka mamlaka ya Usimamizi wa Anga (TCAA) kuanza kufundisha hivyo tunatarajia kuanza kutoaa mafunzo haya mwezi wa sit ana tuanza na wanafunzi kumi na mbili” Alisema Mgaya


 Mwenyekiti wa Bodi Chuo hicho Prof. Ulingeta Mbamba amesema bodi ya chuo hicho kitaendelea kusimamia  Ubora  wa Elimu unaotolewa na chuo hicho kwa masomo yaote ili chuo hicho kiendelee kutoa wataalam wanaoweza kushindana katika soko la ajira za ndani nan je ya nchi.

Mkufunzi wa Mafunzo ya wahudumu wa Ndege amesema kuwa vifaa vyote vya wahudumu wa ndege vipo tayari kwa ajili ya kufundishia hivyo anawakaribisha  vijana   kwenda katika chuo hicho kupata mafunzo ya urubani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI