Header Ads Widget

JKT YAWAITA VIJANA WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2023 KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT

 

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

JESHI la Kujenga Taifa JKT linawaita Vijana wote waliohitimu elimu ya sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2023 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria kwa mwaka 2023.


Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Brigedia Jenerali Hassan Mabena  Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) amesema jeshi hilo la JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo ambapo vijana hao wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia Tarehe 1 Juni Hadi 11 Juni 2023.


Aidha amewataka wahitumu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical Disabilities) kwenda kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo inamiundombinu ya kuwahudumia Watu wa jamii hiyo.


Amesema JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa Kama vile Bukta ya rangi ya' Dark blue' yenye mpira kiununi iliyo na Mfuko mmoja nyuma ,urefu unaoishaia magotini isio na zipu,T- shirt ya rangi ya kijani ,Rabq za Michezo zenye rangi ya kijani au blue,shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahati,Soksi ndefu za rangi nyeusi,Nguo za kuzuia baridi kwa waopangiwa mikoa yenye Baridi,Track suit ya rangi ya kijani au blue,nyaraka zote katika udahili wa kujiunga na Elimu ya juu zikiwemo vyeti vya kuzaliwa ,vyetivya kuhitimu kidato Nne nk Pamoja na nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.


" Orodha kamili ya majina ya vijana hai,makambi ya JKT waliopangiwa na maeneo makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo itapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz ," Amesema Brigedia Jenerali Mabena


Na kuongeza" Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana waliohitimu Kidato cha Sita mwaka 2023 kuungana na vijana wenzao ili kujengewa uzalendo,umoja wa kimataifa ,kufundishwa stadi za kazi ,stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifalao," Amesema 


Amesema vijana hao wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkomo Mara , JKT Msange Tabaora , JKT Ruvu, Pwani JKT Mpwapwa , Makitupora JKT Dodoma, JKT Mafinga Iringa, JKT mlale Ruvuma, JKT mgambo na JKT Maramba Tanga Jkt Makuyuni Arusha , JKT Mulombora , JKT Kanembwa na JKT Mtabila  Kigoma, JKT Itaka Songwe , JKT Luwa na JKT Mikundikwa Rukwa , JKT Nachingwea Lindi, JKT Kibiti Pwani na Olijoro JKT Arusha.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI