Header Ads Widget

RAIS DKT MWINYI MGENI RASMI HARAMBEE YA NISTIRI NISIFEDHEHEKE


NA THABIT MADAI,ZANZIBAR - MATUKIO DAIMA APP

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Harambe ya nistiri nisifedhehe inayoambataka na ukusanyaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa Zanzibar.

Harambe hiyo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mei  mwaka huu katika ukumbi wa Shehe Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni mjini Unguja.

Akizungumza na waandishi wa Habari, katika ukumbi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Mperani Mjini Unguja, Mkurugenzi wa Taasisi ya Asma Mwinyi Foundation, Asma Ali Mwinyi, alisema, mpango huo umekuwa na lengo la kufanya hivyo ni kupunguza changamoto za wanafunzi wanazozipata wakati wakiwa skuli.

Aidha alisema muda mwengine watoto wanakuwa darasani wanakutana na wakati huo na kusababisha kuona aibu na wengine huwa wanakata kwenda skuli.

Alisema,  taasisi yake imeona umuhimu wa kufanya harambee hiyo ili kuwasitiri wanafunzi wa kike kwa kugawa taulo hizo bure kwa wanafunzi wa Zanzibar na kusema kuwa lengo lao hasa kuwapa taulo hizo kwa muda wa mwaka mzima.


"Tutamsitiri bint kwa muda wa mwaka mzima kwani tutampa taulo hizi ambapo mtoto mmoja tutampa paketi 12" alisema

Hivyo, alisema lengo lao ni kuwafikia watoto 6000 wa Skuli za Zanzibar, na kusema kuwa wamekuwa washirikiana na wadau mbalimbali na taasisi za serikali na binafsi ambapo wamekuwa wakishirikiana kuona lengo linafikiwa ikiwemo PBZ

Sambamba na hayo, aliwataka wadau mbalimbali kuendelea kuchangia Harambe hiyo ili kuona lengo linafikiwa la kumsitiri mtoto wa kike.

Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Mohamed Mussa, alisema wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuona wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri ambapo kitendo hicho kuona wanafunzi wanasoma katika mazingira bora

Alisema taasisi ya Asma Mwinyi Foundation, imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuona wanaunga mkono katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu huku akisema serikali inaendeleza jitihada mbalimbali kujenga mazingira ya kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki.

Sambamba na hayo, alipongeza taasisi hiyo kwa kufikiria wazo la kuwasaidia wanafunzi wa kike wanaosoma katika skuli za Zanzibar, kwani wamekuwa ni miongoni mwa wanaounga mkono jitihada za serikali.

Hivyo, aliziomba taasisi nyengine kuendelea kushikana mkono katika kuona jitihada za serikali zinaendelea ambapo wanafunzi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto wakati wa mwenzi kufika.

"Kitendo hichi ni kizuri kwani wanafunzi wakiwa katika kipindi cha hedhi wamekuwa wakipata tabu sana kupoteza hasa muelekeo wakiwemo wanafunzi wa dahalia hivyo harambee hii itasaidia sana kumsitiri mwanafunzi wa kike" alisema.

Nae, Mkurugenzi wa Biashara wa benki ya watu wa Zanzibar, Eddie Mhina, alisema, Benki yao itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali kuona wanasaidia makundi mbalimbali katika shughuli za maendeleo katika jamii.

"Benki yetu inatambua nafasi ya mtoto wa kike na umuhimu wake hasa katika jamii na kumuwezesha mtoto wa kike na kufahamu changamoto wanazozipata katika kipindi cha hedhi, sisi kama benki tutashirikiana na taasisi ya Asma Mwinyi Foundation katika kuchangia harambee hii ili lengo liweze kufikiwa" alisema.

Hivyo, aliwataka wadau kuendelea kushirikiana ili kuwawezesha watoto wa kike na kuahidi kuendelea kuchangia katika shughuli mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI