Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amelaani vikali Kauli iliyotolewa na Jukwaa la wahariri TEF yakwamba mchakato wa marekebisho ya sheria za huduma ya habari ni danadana ambapo ameeleza kauli waliotoa ni kauli ya chuki na za kuvunja moyo.
Amesema ameshangazwa na viongozi hao kutoka na kuongea kwa jaziba mbele ya vyombo vya habari wakati walikuwa pamoja tangu mwanzo
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa Waziri huyo ameeleza, kwa mujibu wa maaelezo yao wamesema mchakato huo umekuwa na danadana na ukisoma na kusikiliza zaidi inaonyesha Serikali imevunjika vipande vipande.
"Kutoka na kwenda Kuzungumza hadharani maneno ya kuvunja moyo sio Jambo la busara na inaleta chuki baina yetu," amesema
Na kuongeza "Tumefanya kazi kwa pamoja tangu mwanzo mwa mchakato huu hadi hapa tulipofikia hivyo basi mashirikiana haya tuendelee nayo hivyohivyo natamani sana tuelewane, "Amesema Waziri Nape
Aidha amewataka kukumbuka kuwa sheria sio ya mtu fulani ni yawatu wote hivyo tuwe na imani zoezi hili litaisha pamoja.
Hata hivyo Jana February 8 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) likisikika likisema limepokea kwa mshituko makubwa kauli ya Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kuwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari (MSA 2016) umeshindikana kuingizwa bungeni kutokana na ripoti nyingi za Kamati za Kisekta za Bunge.
TEF imeona sababu iliyotolewa ni nyepesi na inapata wasiwasi iwapo kuna utashi wa kufanya mabadiliko katika sheria hii.
Aidha wamesema Katika vikao vilivyotangulia, waliona ugumu kutoka kwa baadhi ya maofisa wastaafu walioazimwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,na baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama wakionesha wazi kutokuwa na nia ya kurekebisha sheria hii.
Wamesema Mara kadhaa vikao vilivyofanyika, viliisha bila mwafaka katika vifungu mbalimbali ikiwamo Mamlaka ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) chini ya vifungu vya 9 na 10, ambavyo vinampa mamlaka ya kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka, mtoa hukumu na msimamizi wa utekelezaji wa hukumu;suala tunalosema ni ukiukwaji wa Utawala Bora na Utawala wa Sheria.
0 Comments