Header Ads Widget

NTIBENDA KIJIKO AIBUKA MSHINDI MJUMBE BARAZA KUU TAIFA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA KIGOMA

 



Na Editha Karlo,Kigoma

 Matokeo ya uchaguzi wa mjumbe wa baraza kuu Taifa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Kigoma.


Wagombea katika nafasi hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye ofisi za chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mkoa wa Kigoma tarehe 7 mwezi pili walikuwa watatu ambao ni Dkt Daudi Felix Ntibenda,Dkt Khamed Sovu na Ndugu Mganza.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi katibu wa Wilaya ya Kigoma mjini Zaibu Kasimba alisema Dkt Felix kibenda alipata kura 20 huku Dkt Khamad Sovu akipata kura 19 na ,Bwana mganza amepata kura 2.


Baada ya kutangaza matokeo hayo uchaguzi ulirudiwa tena kwa wagombea wawili tu  Dkt Felix Ntibenda na Dkt Khamad sovu ambapo baadae Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;

Dkt Daudi Felix Ntibenda Kijiko alipata kura 22 na Dkt Khamad Sovu amepata kura 18 baada ya hapo Msimamizi wa uchaguzi alimtangaza Dkt Daudi kuwa mshindi wa nafasi hiyo.


Akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo baada ya uchaguzi mshindi Dkt Daudi Felix Ntibenda Kijiko alisema uchaguzi umeisha hakuna makundi tena sasa kazi iliyobaki ni kuijenga jumuiya ya wazazi ili iwe imara.


"Ninawashukuru wajumbe kwa heshima mliyonipa ya ushindi huu,ninawahaidi tutafanya pamoja kwa kushirikiana ili kujenga jumuiya yetu,makundi ya uchaguzi tuyavunje tubaki tuwe kitu kimoja na kazi iendee"alisema Kijiko


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI