Header Ads Widget

MWENYEKITI MPYA UVCCM MBINGA AWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDO

  

Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya ya Mbinga Herswida Komba akiongoza zoezi la upandaji miti.

Na Amon Mtega, Mbinga

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana  wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Herswida Komba amewataka Vijana wa Wilaya hiyo kuendelea kuwa wazalendo wa Jumuiya hiyo  ili Taifa liendelee kusongambele kimaendeleo.


Komba ametoa wito huo wakati akizungumza na Vijana wa Wilaya hiyo katika kata ya Ngima wakati wa kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM  ambayo kilele chake kitakuwa Februari tano mwaka huu.


 Mwenyekiti huyo  ambaye aliongozana na kamati yake mpya ya utekelezaji huku naye ikiwa ni mara yake ya kwanza kuongoza tukio hilo tangu achaguliwe hivi karibuni amesema kuwa Vijana ndiyo tegemeo la Taifa hivyo inatakiwa kuendelea kuwa wazalendo wakuipenda Jumuiya yao pamoja na Taifa.


Hata hivyo mwenyekiti mpya huyo akiwa katika kata hiyo ameongoza zoezi la upandaji miti katika shule ya Sekondari ya Ngima ambayo inaendelea kujengwa haijakamilika , upandaji wa miti katika ofisi ya tawi la CCM la Pandisa lililopo katani hapo pamoja na kufualia zoezi la usajili wa wanachama kwa njia ya kielektroniki (Tehema)ili kila mwanachama taarifa zake ziwe kwenye mfumo.


Pia akiwa katika Sekondari hiyo na kupokea taarifa ya ujenzi wa shule mwenyekiti huyo amesema kuwa lazima kujitahidi kukamilisha ujenzi huo ili watoto waweze kupatiwa Elimu kwenye shule hiyo huku akiwaomba Vijana kuipongeza na kuisema Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miradi mbalimbali inayofanyika.


Kwa upande wake katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbinga Mohamed Salumin amesema kuwa Vijana wa Wilaya hiyo wamejipanga vema na kuwa hadi sasa zoezi la usajili wa wanachama kwa sekta ya Vijana linaenda vizuri hadi sasa wanachama 39 wamesajiliwa na zoezi kinaendelea.


 Naye katibu Hamasa na Chipukizi wa Wilaya hiyo Daniel Nkoma amesema kuwa Vijana wapo tayari kushirki shughuli mbalimbali za kijamii  ikiwemo kupita kwenye shule za msingi na Sekondari kuanzisha matawi ambayo yatakayojikita kuwafundisha Vijana kuwa wazalendo wakuipenda Nchi yao.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS