Header Ads Widget

WAZIRI WA ELIMU WA GAMBIA AFURAHISHWA NA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA VETA

Na Fatma Ally Matukio na Habari App

Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia na Utafiti kutoka Serikali ya Gambia, Prof. Pierre Gomez ametembelea banda la (Veta) lililopo katika viwanja vya Julius Nyerere (Sabasaba) ambapo ameridhishwa na kazi mbalimbali zinazofanywa na wabunifu kutoka Veta.

Akizungumza mara baada ya kukagua banda hilo amesema kuwa amevutiwa na Sanaa za mikono zilizofanywa na wabunifu wa mikono ikiwemo, kuchonga vitu mbalimbali kwa kutumia vifuu, mashine za mbao za kukatia chupa na kutengeza thamani ikiwemo glass.

"Nilivyopita kwenye banda hili nimependa zaidi Sanaa za mikono zilizotengenezwa kwa ubunifu mkubwa hivyo amefurahishwa sana kwani wametumia vitendo zaidi kuliko nadharia"amesema Prof. Gomez 

Amesema kuwa, wanafunzi wa Veta wametumia ubunifu mzuri sana katika kuzalisha bidhaa zao na zinavutia jambo ambalo linawajenga zaidi kufanya kazi kwa vitendo kuliko nadharia.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA Antony Kasore amesema mafunzo yanayotolea ni muhimu sana mpaka yanapelekea mtu kujiajiri na kuanza kufanya shughuli za ujasiliamali na pia wameona wafunzo ya veta yalivyojikita kwa vitendo zaidi kuliko nadharia

Ameongeza kuwa, kwao ni faraja kumpokea Prof Gomez kwani wamekuja kujifunza mafunzo ya elimu na pia kujione maswala mbalimbali yanayofanyika kuhusiana na sayansi na techolojia pamoja na ubunifu nchini.

"Leo amekuja kwenye maonyesho ya  49 kimataifa ya biashara ( Sabasaba) ili kuangali Taasisi zote zilizopo chini ya wizara ya elimu jinsi zinazofanya kazi zake na wameweza kuona vitu mbalimbali vinavyofanywa na veta kuanzia kwenye utoaji wa mafunzo, kwenye ubunifu mpaka mwisho wa siku kuweza kuwafundisha watu ujasiliamali" amesema CPA Kasore

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI