Header Ads Widget

RC APONGEZA JITIHADA ZA KUWAINUA VIJANA ZINAZOFANYWA NA MWEKEZAJI WA ZAO LA VANILA.

 

 NA THABIT MADAI, ZANZIBAR – MATUKIO DAIMA APP

 MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Hadid amepongeza jitihada mbalimbali za kuwainua Vijana zinazofanywa na Mwekezaji wa Kilimo cha Vanilia katika Eneo la Bungi Mkoa wa Kusini Unguja na kuwataka Wananchi kujitokeza kuwekeza katika zao la Vanila ambalo linatajwa kuwa zao lenye Tija Duniani.

 

Pongezi hizo amezitoa leo wakati wa ziara maalum ya kukagua Uwekezaji Katika Kilimo cha Vanila na Vitungu huko Bungi Mkoa wa Kusini Unguja ambapo Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kutokana na Maendeleo yanayofanywa na Mwekezaji huyo katika kilimo cha Vanila amefarijika na kuona vijana wengi ndani ya mkoa huo wamepata ajira na kujikwamua kimaisha.

 

Ameeleza kuwa zaidi ya vijana 200 wamepata ajira katika kilimo cha Vanila na kujikwamua kiuchumi.

 

“Ukweli kuwa nimefarijika kuona vijana wetu ndani ya Mkoa wa Kusini wamepata ajira ya kupitia kilimo cha Vanila ambacho ni kilimo cheenye faida Duniani,” ameeleza.

 

Aidha ameeleza kwamba, hadi sasa bado hawajapokewa changamoto kutoka kwa Wananchi na Wakulima juu ya Mwekezaji huo.

 

Amesema Wananchi wanapaswa kutokuwa na Wasiwasi juu ya Uwekezaji wa Zao la Vanila na Vitunguu katika eneo hilo kwani Serikali ndani ya Mkoa huo ina wasimamia Wawekezaji mbalimbali na kuhakikisha wanatenda haki kwa Wananchi.

 

“Wananchi wanapaswa kutokuwa na Wasiwasi, Serikali inapaswa inawafuatilia kwa kina wawekezaji wake na endapo watabaini kuwa na changamoto zozote zile huwa wanachukua hatua,”Amesema.

 

“Hadi sasa bado sijapata Kesi ya kuwa Vijana wana Shida katika utekelezaji wa Mradi na Kilimo cha Vanila hivyo Serikali ipo karibu na wawekezaji ili kubaini kama kuna changamoto yoyote ile na kuweza kuitatua,” ameeleza.

 

Hata hivyo ametoa Wito kwa Wawekezaji kujitokeza kuweza Kuwekekeza katika Maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja katika Miradi ya Kilimo, Uvuvi na Uchumi wa Buluu.

 

“Nichukue Fursa hii kuwataka wawekezaji wa ndani na Nje kujitokeza katika kuwekeza katika Kilimo na Sekta mbalimbali lakini pia kuhakikisha wanatenda haki kwa Wananchi na vijana wanaotekeleza miradi yao,” ametoa wito.

 

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vanila International amepongeza ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa wa Kusini Unguja katika eneo hilo na kuomba kuongeza mashirikiano na Serikali katika kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo.

 

“Sisi Vanilla Internationa tunatekeleza Miradi mbalimbali ya Kilimo cha Vanila, Vitunguu na Ufugaji hivyo tunaomba kuongeza Mashirikiano na Serikali ili Mradi hii kuendelea kuwanufaisha Wananchi mbalimbali visiwani hapa,” ameeleza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS