Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali,Twalib Lubandamo
Na Matukio daima media, Mbarali
ASILIMIA kubwa ya utelekezaji wa watoto katika halmashauri ya wilaya
ya Mbarali mkoani Mbeya unatokana na unyanyasi wa wanaume kwa
wanawake ambao hutokana na vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa
vikiendelea kufanywa na kupelekea kutekeleza familia zao .
Wilaya ya Mbarali imekuja na mwarobaini wa changamoto hiyo ambapo
uongozi uongozi wa halmashauri hiyo umepanga kukabiliana na tatizo
hilo kwa kutembea kata , vitongoji ,vijiji kuangalia kiini cha
tatizo hilo na kupata suluhisho na tatizo hilo kuisha kabisa .
Hayo yammesemwa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mbarali
mkoani Mbeya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Itamboleo, Twalib
Lubandamo wakati wa kikao cha mkutano wa kawaida wa
baraza la madiwani wilayani humo uliofanyika jana katika ukumbi wa
Maji.
Lubandamo amesema kuwa kero kubwa ambayo anakutano nazo katika ofisi
yake ni ugomvi wa ndoa na familia zilizotelekezwa na kusema mpaka
sasa analea familia sita zilizotelekezwa .
‘’Nina mtoto mwingine ambaye nimemchukua Igurusi Sekondari yupo
vizuri sana kimasomo ambaye amepata ufaulu mzuri sana kwenye matokeo
yake ya kidato cha Nne ,ninao watoto wengi ninaolea sisi wanaume
tumekuwa wanyanyasi wakubwa kwa wanawake hivyo wanawake wanaenda
kupata shida na watoto kwa hiyo kero nyingi tulizo nazo asilimia
kubwa ni wanawake kuja na familia zao na ugomvi wa ndoa unakuta muda
mwingine mwanamke anakuja kapigwa mpaka katolewa sikio kung’atwa ulimi
kwakweli wanaume tumekuwa wakatili sana ,wiki iliyopita alikuja Mama
mmoja na watoto sita hawajala chochote hivyo ilibidi kama halmashauri
tujichange kumsaidia mama huyu ‘’amesema Mwenyekiti huyo wa
halmashauri .
Akizungumzia zaidi Mwenyekiti huyo amesema kama halmashauri
wamejipanga kwa kukabiliana kuwa kila kijiji , kitongoji kuanzia
Mwezi marchi kwenda kuangalia changamoto za wanawake na kuhakikisha
zinakwisha moja kwa moja.
Kaimu Mganga mkuu Halmashauri ya wilaya ya Mbarali idara ya afya na
ustawi wa jamii na lishe , Dkt.Ray salandi amesema kuwa kitengo cha
ustawi wa jamii kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha walikuwa na jumla
ya migogoro ya kifamilia 334 ambapo kwa asilimia kubwa migogoro
hiyo imetokana na ukatili wa kimwili kwa maana ya vipigo ambavyo
vinafanya jumla ya vipigo 113 ambayo ni sawa na asilimia 34
iliyosuruhishwa kwa kipindi cha robo ya pili.
Hata hivyo Dkt. Salandi amesema changamoto nyingine kubwa ni matunzo
kwa watoto ambapo kulikuwa na familia 106, zilikuwa na changamoto ya
matunzo kwa watoto na kufan ya kufanya asilimia 32 hivyo kwenye
idara hiyo wameendelea kutatua changamoto na migogoro 334 ,ilifika
kikomo kwa kufuata taratibu za kisheria ikiwemo polisi.
Diwani wa Kata ya Miyomboni ,Jeremiah Kisangai amesema utelekezaji
watoto unasabishwa na wanaume kuingia kwenye mahusiano na kusabisha
mimba zisizotarajiwa kwa asilimia kubwa kama halmashauri zoezi
lilishafanyika la kuwapitia na kupatikana kwa mashauri mengi zaidi
ya 300.
Kisangai amesema kuwa baada ya kuyapitia walibaini vitu vingi lakini
kubwa halmashauri imejipanga kwenye maeneo ya vijiji kuna kamati
zinazoshughulikia kukaa kila wakati kushughulikia kero hizo ili
kupunguza matatizo hayo hususani Madiwani .
0 Comments