UMOJA wa wanawake Tanzania (UWT) mkoani Iringa umesema kutokana na uongozi bora ulionyeshwa na serikali ya awamu ya sita pamoja na utekelezwaji mzuri wa Ilani ya chama hicho kwa pamoja umeamua kuwa utamchukulia fomu ya kugombea Urais 2025, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili kuweza kukamilisha yale yote ambayo yatakuwayamesalia katika kuwatumikia Watanzania.
Hayo yamesemwa na katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Rukia Mkindu ambayealimwakilisha wa mgeni rasmi MNEC Salim Abri Asas katika kikao Cha baraza kuu la UWT mkoa wa Iringa lililofanyika Ukumbi wa CCM mkoa .
"Katika kuhakikisha kuwa yale alitoyaanzisha Mama yetu mpendwa Mama
Samia yanakamilika, sisi kama CCM Iringa tumejipanga kumchukulia fomu
ya ugombea Urais na kuigharamia kwa 100%..." Alisema.
Asas alimewataka akina mama wa mkoa wa Iringa kuitumia mikopo inayotolewa na serikali
ya awamu ya sita ili iwasaidie kuwainua kiuchumi kwani ni kwa ajili
yao.
"Mikopo inayotolewa na awamu ya sita ni kwa ajili yetu akina mama,
tuitumie kutunufaisha na kutuinua kiuchumi. Bahati nzuri mikopo ya
kipindi hiki sio mikopo kiduchu, ni mikopo ya kututoa kwenye wimbi la
umaskini kama tutaitumia vizuri"
Awali akifungua kikao hicho mwenyekiti wa umoja wa wanawake mkoa wa
Iringa Zainabu Mwamwindi amewataka kushikimana kwa pamoja katika
kipindi hiki ambacho uchaguzi umekwisha ili kuweza kuwatumikia
wananchi kwa ngazi zote.
"...Katika kipindi hiki ambacho hatuna uchaguzi na tunajiandaa kwa
chaguzi zijazo, ni wakati wa sisi kukijenga chama chetu katika nyanja
zote kupitia jumuiya zetu za wazazi, wanawake na vijana ili tufanye
vizuri katika uchaguzi ujao.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego alisema umoja wa wanawake
Tanzania (UWT) unakuwa kioo kwa wanawake wengine ambao wapo nje ya
umoja huo pamoja kuwasaidia katika kutatua changamoto zao kwa
kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.
0 Comments