Header Ads Widget

HALMASHAURI KIGOMA ZATAKIWA KUAJIRI WATUMISHI SEKTA YA AFYA

 

      Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Halmashauri za mkoa huo zimetakiwa kutengeneza mipango na kuajiri watumishi wa sekta ya afya  kwa kutumia mapato ya ndani ili kukabili upungufu mkubwa wa watumishi wa afya uliopo mkoani Kigoma.

Katibu tawala mkoa wa Kigoma,Hassan Rugwa ametoa maelekezo hayo kwa halmashauri za mkoa Kigoma   wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Songambele wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Rugwa alisema kuwa kwa sasa mkoa Kigoma unakabiliwa na upungufu wa watumishi  1561 ambao ni wakunga na wauguzi  idadi ambayo inaelezwa kutoendana na ikama ya wagonjwa pamoja na ongezeko la vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Kigoma.

Kutokana na changamoto hiyo Katibu Tawala huyo wa mkoa Kigoma alitoa wito kwa Halmashauri za mkoa Kigoma kuongeza mapato katika ukusanyaji wa mapato yake ya ndani lakini muhimu Zaidi kutumia mapato hayo kutengeneza mpango ambao utaziwezesha halmashauri hizo kuajiri watumishi wa idara ya afya na kuwalipa kutumia mapato ya ndani ili kupunguza upungufu huo wa watumishi.


Akizungumza katika maadhimisho hayo Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma,Damas Kayera alisema kuwa kumekuwa na maboresho makubwa ya majengo na miundo mbinu katika sekta ya afya mkoani Kigoma sambamba na ujenzi wa majengo mapya ya kutolea huduma lakini maboresho hayo hayaendi sambamba na upatikanaji wa watumishi hivyo sektaa ya afya mkoani Kigoma kukabiliwa naa upungufu mkubwa wa watumishi.

Pamoja na hilo Kayera alisema kuwa watumishi hao kupitia idara na vitengo wamekuwa wakijipanga kuhakikisha huduma zinazotolewa kikamilifu lakini pia wakati mwingine watumishi hao kufanya kazi kwa masaa mengi ili kuhakikisha huduma zinafanyika  ikiwemo kupambana na vifo vya mama wajawazito na watoto.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI