Header Ads Widget

WANANCHI KIGOMA WAPOKEA MABEHEWA MAPYA KWA SHANGWE

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma



Mamia ya wananchi wa mkoa Kigoma wamejitokeza kwa wingi  kwenye stesheni ya reli ya Kigoma kwa ajili ya  mapokezi ya treni yenye mabehewa ya kisasa yaliyonunuliwa na serikali hivi karibuni.



Akizungumza muda mfupi baada ya treni hiyo kuwasili stesheni ya Kigoma Mbunge huyo wa Kigoma mjini,Kilumbe Ng'enda  ameishukuru serikali kwa kusikiliza kilio cha wananchi kwa kuboreshwa kwa miundo mbinu ya treni ikiwemo vichwa vya treni na  mabehewa.



Ng'enda alisema kuwa kwa muda mrefu akishirikiana na wabunge wenzake wa mkoa Kigoma wamekuwa wakipiga kelele kuhusu suala la treni ikiwemo kuongezwa kwa mabehewa ya kisasa.


Amesema kuwa kuboreshwa kwa usafiri wa treni kuna maana kubwa kiuchumi, kibiashara na maisha ya wananchi wa mkoa Kigoma kwa jumla hivyo wanamshukuru Raisi Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa jambo hilo.




Akizungumza mjini Kigoma muda mfupi baada ya kuwasili na treni hiyo Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji TRL, Focus Makoye alisema kuwa jumla ya mabehewa 21 yamesafiri na treni hiyo yaliyonunuliwa na serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 22.


Alisema kuwa treni hiyo itakuwa inatoka Dar es Salaam Jumatatu na kufika Kigoma Jumanne na kuondoka Kigoma kila jumatano huku nauli yake ikiwa Sawa na treni ya Delux.



Makoye alisema kuwa ununuzi wa mabehewa hayo ni mpango wa serikali kupitia shirika ⁿ99njia reli na kwamba maboresho zaidi yanaendelea kufanyika kwa treni zote ikiwemo treni iendayo kasi (SGR).



Pamoja na hilo alisema kuwa watazingatia utoaji huduma bora na usafi na hivyo kuomba wananchi kuzingatia taratibu zinazotolewa na shirika.


Baadhi ya wananchi waliosafiri na treni hiyo akiwemo Prisca Emanuel ambaye alisema kuwa treni imekuwa na huduma nzuri na wamefurahia kusafiri na treni hiyo.





Kwa upande wake Salum Maftah mkazi wa Ujiji mjini Kigoma alisema kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Kigoma wanapenda kusafiri na treni kwa sababu ni usafiri wenye gharama nafuu na usio na usumbufu kama mabasi hivyo wameomba kuimarishwa kwa usafiri huo na kumpongeza Raisi Samia kwa ununuzi wa mabehewa hayo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI