Header Ads Widget

JAMII YATAKIWA KUBADILISHA MITAZAMO HASI ILI KUPUNGUZA VITENDO VYA KIKATILI

 


NA HAMIDA RAMADHAN ,DODOMA


JAMII inapaswa kubadili mitizamo hasi ambayo imekuwa ikichochea kwa kiasi kikubwa vitendo vya kikatili wa kijinsia ikiwemo Ulawiti,ubakaji na mauaji ya wenza ambayo vimekuwa vikiongezeka kila siku.


Ofisa program mwandamizi wa Mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) Zainab Mmary, alibainisha hayo jijini hapo katika kikao kazi cha watendaji wa serikali kuu.


“Bado matukio ya ukatili nchini yanaongezeka kila siku lakini kwa kaiasi fulani tunapiga hatua lakini moja ya changamoto iliyopo ni jamii zetu kubadili mitizamo kwani hata mfumo dume bado ni sababu ya watoto wetu kulawitiwa kwani mwanaume anachokitaka ni lazima akipate kwa ghalama yoyote ile,”alisema



Aidha, alisema pamoja na matatizo yaliyopo, lakini angalau hivi sasa jamii imeanza kubadilika kiasi kwa kujitokeza kutoa taarifa za vitendo hivyo vya ukatili katika vyombo mbalimbali.


“Zamani ilikuwa vigumu sana matukio haya ya ukatili kuzungumzwa wazi katika jamii kama vile binti kubakwa ilikuwa ni vigumu sana kusema au mtoto kulawitiwa”alisema


Kadhalika, aliishauri serikali kuenmdelea kutoa elimu kwa jamii ili kubadili tabia ikiwa ni pamoja na kuwezesha wananchi kiuchumi kwakuwa watu kukaa bila kazi ya kufanya ni moja ya sababu ya kuongezeka kwa matukio hayo.


“Harakati tunazozifanya zimetiliwa mkazo sana lakini bado kuna ombwe kubwa la rasilimali fedha hata tatizo likitokea sehemu fulani watu wanakosa uwezo wa kufika kwa wakati”alisema


Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Makundi maalum, Simon Magesa alisema licha ya uwepo wa sheria kali lakini bado vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto vinaendelea.



“Kuna sheria ambayo inasema kuwa kama mtu akimbaka mtoto chini ya miaka kumi anafungwa maisha lakini akimbaka mtoto wa zaidi ya miaka kumi ni kifungo cha miaka 30 lakini bado watu wanafanya matukio haya sasa inabidi tuangalie na tatizo la afya ya akili katika jamii zetu ili kuchukua hatua na kumaliza tatizo hili kwani ni jambo la kushangza mzazi kumlawiti mtoto wa kumzaa mwenyewe”alisema Magesa


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI