Header Ads Widget

SIRO AITAKA KAKONKO KULIMA KIBIASHARA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Saimon Siro ameitaka Halmashauri ya wilaya Kakonko mkoani Kigoma kutumia fursa ya kuwepo mpakani na nchii za Burundi na jirani ya Rwanda kuongeza uzalishaji wa mazao kuyafanya ya biashara ili  kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo na nchi kwa jumla kutokana na soko la uhakika la mazao lililopo kwa nchi hizo.

Balozi Siro alisema hayo alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo ambapo alisema kuwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya kilimo utachochea maendeleo makubwa ya kiuchumi ya wananchi wa wilaya hiyo.

Alisema kuwa wilaya ina eneo kubwa linalofaa kwa kilimo ikiwa na rutuba ya kutosha na wananchi wanayo ari ya kufanya kilimo biashara hivyo Halmashauri inapaswa kuweka mipango ambayo itawaunganisha wananchi hao na fursa za kuongeza uzalishaji zinazoenda sambamba na fursa ya masoko.


Akizungumza katika kikao na viongozi na watumishi wa wilaya hiyo alitoa maelekezo kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha mpango wa kilimo cha mashamba makubwa ya parachichi, mihogo, maharage na mahindi unasimamiwa vizuri kwani uzalishaji wa mazao hayo una fursa kubwa kuchochea uchumi wa wilaya hiyo.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kakonko,Stephen Ndaki alisema kuwa halmashauri hiyo imepania kuongeza maradufu ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia kilimo na shughuli za biashara.


Ndaki alisema kuwa kwa sasa wameanzisha shamba la Hekari 1500 kwa ajili ya kilimo cha Parachichi ambalo wamepata soko la zao hili lakini pia kwa sasa wana mtandao wa kuuza mazao katika nchi za Burundi,Rwanda, kenya na Sudan Kusini huku wakiimarisha vibanda vya biashara katika soko la wilaya Kakonko la stendi kuu ya mabasi ya wilaya hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI