Header Ads Widget

TUZIDI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA KATIKA KUDUMISHA AMANI YETU – JASMIN NG’UMBI

 


Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

MUFINDI

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jasmin Ng'umbi, amewataka Watanzania kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuhakikisha taifa linabaki kuwa la amani, mshikamano na utulivu.


Akizungumza na Matukio Daima Media Jasmin ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mufindi, alisema kuwa Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha amani kutokana na juhudi kubwa na maono ya Rais Samia katika kulinda misingi ya umoja wa kitaifa.

Alisema ipo haja kwa kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake kushiriki kwa vitendo katika kuilinda amani iliyopo kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali, huku akiwataka vijana kuwa mstari wa mbele kutetea mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya awamu ya sita.

"Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhimiza maridhiano, mshikamano, demokrasia na maendeleo. Ni wajibu wetu kama raia wema kuhakikisha tunamtia moyo na kumuunga mkono kwa vitendo. Amani si jambo la kubahatisha, ni matokeo ya kazi kubwa ya viongozi wetu wakiongozwa na Rais Samia," alisema Jasmin.

Akiwaasa Watanzania kuendelea kuwa watulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Jasmin alisema kipindi cha uchaguzi si wakati wa kupandikiza chuki au uhasama bali ni muda wa kujenga hoja na kushindana kwa sera zenye mashiko zitakazoinua maisha ya wananchi.

"Tupo katika kipindi nyeti kuelekea uchaguzi, ni lazima tuendelee kuiheshimu na kuilinda amani yetu. Kuna baadhi ya watu kutoka vyama vya upinzani ambao kwa makusudi wanapandikiza taharuki na kutamani kuona amani hii inatoweka. Watanzania wasikubali kugawanywa. Nchi hii ni yetu sote," alisema Jasmin.

Aliongeza kuwa historia inaonesha namna Tanzania imekuwa mfano bora wa kuigwa barani Afrika kwa utulivu wake hata wakati wa mabadiliko ya kisiasa, jambo linalotakiwa kulindwa na kila Mtanzania kwa gharama yoyote.

Jasmin pia alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana wa UVCCM na Watanzania kwa ujumla kuwa mabalozi wa amani, kuhakikisha ujumbe wa mshikamano unafika kila kona ya nchi ili uchaguzi uwe wa amani, huru na haki.

Hata hivyo Jasmin alisema  kuwa kama Taifa linataka kufikia maendeleo ya kweli, lazima liendelee kuwa na amani na maridhiano ya kitaifa, akibainisha kuwa hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana pasipo utulivu na mshikamano miongoni mwa wananchi.

“Tuendelee kumuombea Rais wetu, tumtie moyo na tushikamane katika kulinda misingi ya nchi yetu. Tuwe sehemu ya amani, si chanzo cha vurugu,” alihitimisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI