WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCMNEC) Mkoa wa Pwani.
Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji alishinda katika uchaguzi wa CCM Mkoa uliofanyika Kwa Mathias Mjini Kibaha.
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Zainabu Telaki alisema mshindi alipata kura 762.
Alisema kuwa kura zilizopigwa ni 834 zilizoharibika ni 6 kura halali zikiwa ni 828 ambapo mshindi wa pili alikuwa Mbaraka Dau aliyepata kura 38, Abihudi Shila alipata kura 12, Nunu Mkanza alipata kura 11 na Mohamed Mtuliakwao alipata kura 5.
Aliwashukuru wajumbe na kusema kuwa wamempa imani kubwa kura walizompatia atahakikisha wanasimamia vema miradi ya chama ili ikamilike kwa wakati ilete maendeleo kwa wananchi.
0 Comments