Header Ads Widget

MWENYEKITI LEKULE "MJI MDOGO WA HIMO UPO KISHERIA NA UNATAMBULIKA"



 Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

MWENYEKITI wa Mamlaka ya mji mdogo wa Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, Robert Lekule amesema kuwa mji huo upo kisheria na unatambulika na Serikali japokuwa unalelewa na Halmashauri ya Moshi.



Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo katika Baraza la mamlaka lililofanyika leo akijibu swali la papo kwa hapo lililoulizwa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Zilipenda, Hassan Msangi ni vigezo vipi vimebakia kutekelezwa ili mamlaka ya mji mdogo wa Himo iwe mamlaka kamili inayojitegemea 



Lekule alisema kuwa, kwa mujibu wa Sheria mamlaka zote zinalelewa chini ya Halmashauri ya eneo husika na kuwataka wajumbe kutambua kuwa mji wa Himo umeshatimiza vigezo vyote na ndio maana ni mamlaka kamili ya mji mdogo.



Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwa sasa imefika haha wajumbe kujipanga kuomba mji mdogo huo wa Himo kupandishwa hadhi na kuwa Halmashauri kwani hata eneo lililopo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 92 inastahili kuwa Halmashauri.



"Wajumbe tunapaswa kujipanga kuomba Halmashauri yetu ya Himo kwani inakilomita za mraba 92 ili tuweze kujitegemea wenyewe bila kulelewa na Halmashauri ya Moshi"  alisema Lekule.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI