Header Ads Widget

MATOKEO YA UCHAGUZI CCM MKOA WA IRINGA,YASSIN AULA UENYEKITI MKOA ,ASAS MNEC TENA


Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Arif Abri katikati akimpongeza MNEC Salim Abri Asas Kwa Ushindi wa asilimia 92.
.............

WAJUMBE  wa  mkutano mkuu  wa  uchaguzi wa  chama  cha mapinduzi (CCM)  mkoa wa  Iringa  wamemchangua  Daud  Yassin kuwa  mwenyekiti  wa mkoa huo  huku  Salim Abri  Asas akitetea nafasi yake  kwa  kupata  kura 593  sawa na asilimia 92.


Akitangaza  matokeo hayo jana   msimamizi mkuu  wa  uchaguzi  huo kanali  Laban  Thomasi alisema  kuwa  kwa  upande  wa  uenyekiti  wagombea  walikuwa  watatu  ambapo  Daud Yassin alishinda  kwa  kupata  kura 481  kati ya  kura  651  zilizopigwa   huku Dkt Neema  Chaula  akifuatia kwa  kupata  kura 122 na Anna Mlalambia akipata  kura 48.


Katika nafasi ya Halmashauri  kuu ya  CCM Taifa (NEC) akiwakilisha  mkoa  wa Iringa  wagombea walikuwa watatu  ambao  aliyekuwa MNEC  kipindi  kilichopita  Salim Abri  Asas akifanikiwa  kutetea nafasi yake  kwa  kupata  kura  593  sawa na  asilimia 92  ya  kura  halali 645  huku  akiwashinda wapinzani  wake  Mgambe  Kihongosi  aliyepata  kura 34 na Dkt. Alex Elia Sanga akipata  kura  18.

 



Kwa  upande wa  nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa ambapo kuna nafasi mbili kila wilaya kwa Wilaya ya Kilolo ni Seki B. Kasuga  alishinda  kwa  kupata  kura  513  huku  wa  pili  akiwa ni Leah V. Mwamoto aliyepata kura 340

 

 Wilaya ya Mufindi ni Dickson H. Mwipopo aliyepata kura 480 na  Godfrey Mosha aliyepata kura 246, Wilaya ya Iringa Vijijini ni Christopher S. Mahembe aliyepata kura 309 na Kanuth T. Mhongole aliyepata kura 212 na Wilaya ya Iringa Mjini ni Tumaini G. Msowoya aliyepata kura 488 na Vitus S. Mushi aliyepata kura 297.







































Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI