Baadhi ya waathirika wa sakata la kutumia vyeti vya kughushi mkoani mbeya walioondolewa katika vituo vyao vya kazi wameeleza changamoto walizokutana nazo mara baada ya kufutwa kazi kutokana na changamoto hiyo.
Wakizungumza baada ya serikali kutangaza kuwalipa sehemu ya fedha zao walizochangia katika mifuko ya hifadhi za jamii, wamesema baada ya kuondolewa kazini walipitia maisha magumu na changamoto mbalimbali ikiwemo kuugua kutokana na kukosa fedha walizokua wakitegemea kuzipata ikiwemo mafao ya kustaafu.
Itakumbukwa kwamba mapema hii Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako akiwa jijini Dodoma, alitangaza maamuzi ya serikali ya kuwalipa watumishi hao ambapo watalipwa zile asilimia walizochangia katika mifuko hiyo ya hifadhi za jamii.






0 Comments