Vijana wametakiwa kushiriki kikamilifu katika fursa mbalimbali za kimaendeleo zilizopo na zinazoletwa na serikali pamoja na wadau wa maendeleo mkoani Mtwara.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)kwenye ufunguzi wa Mradi wa vijana kwanza ulio chini ya taasisi ya DOOR OF HOP mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abasi amesema kuwa mkoa wa Mtwara umekuwa na fursa mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo uwepo wa gesi asilia Bandari ,utalii ,uvuvi na kilimo ambazo vijana wazawa wanaweza kuwezeshwa na kushiriki kikamilifu ili kuboresha viwango vya maisha na kuchangia pato la taifa kwa ujumla wake.
Aidha Kanali Abas ameomba ushirikiano kwa mashirika mengine kuja mtwara kusaidia katika sekta mbalimbali kama vile Elimu,afya pamoja na jinsia ili kuijengea uwezo jamii kwa ujumla na kuondoa msongo wa mawazo kwa vijana.
Pia RC Abasi ameyataka mashirika mengine yaliyopo mkoani Mtwara kuya angalia upya kwa kuyahakikiki na kama hayata kidhi vigezo yapunguzwe ili kuayaacha yale yenye tija kwa serikali na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa DOOR OF HOP Tanzania Clemence Clelinus Mwombeki amesema kuwa mradi wa vijana kwanza umelenga kukuza nafasi za vijana kushiriki masuala ya umma na kuwajengea uwezo na uwezeshaji wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kuondoa changamoto ya migogoro iliyopo katika maeneo mbalimbali kwenye mkoa wa mtwara pamoja na kuwajengea uwezo vyombo na tasisi za umma ambazo zimekuwa zikishirikiana vizuri na vijana ili mwisho wa siku ushirikiano kati ya serikali na vijana yakuzwe na kuimarisha ili vijana wapate maeneo yanayoweza kupeleka changa moto yao.
Pia Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuna masuala ambayo wanatakiwa kuyaeekea nguvu zaidi ambayo yameibbanika katika Halmashauri sita zilizopo mkoani Mtwara ikiwepo masuala ya kijinsia ambayo imeendelea kuwa changamoto katika jamii nyingi huku matarajio ya Mradio huo nikuona jamii yenye vijana wenye maana,kuzalisha ,taarifa sahihi za nchi yao ,wazalishaji nammwisho wa siku kuongeza chachu na jitihada kubwa zielekeze kwao ili kuliisadia taifa ikiwa ni kundi kubwwa kwenye jamii .
Nae Ever Samson Nyange kijana kutoka kjiji cha Kilambo Halmashauri ya Wilaya Mtwara amesema kuwa mradi utaweza kusaidia kwa asilimia kubwa kuondoa changamoto zilizopo kwa vijana ikiwepo ukatili wa kijinsia wanaotendewa hususani kwa vijana wa kike ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa vitendo hivyo.
Kwa upande wa Jamali Amiri kijana kutoka Wilayani Masasi amesema kuwa kumekuwa na vitendo vya ukatili unaoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali ya Mtwara ambao huenda ikawa inasababishwa na vijana kutopewa Elimu ya kujitambua na kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao hivyo kupitia dhima ya mradi huo utawezesha kuondoa vitendo hivyo kwa Elimu watakayo ipata .
Mradi wa kijana kwanza upo chini ya shirika la DOOR OF HOP Tanzania unaofadhiliwa na USAID ambao unatekelezwa kwenye kata 13,vijiji 51 kwenye Halmashauri tano zilizopo mkoa wa Mtwara wenye lengo la kukuza nafasi za vijana kushiriki katika masuala ya umma na kuondoa migogoro iliyopo katika maeneo ambayo vijana wanashindwa kupeleka changamoto zao.







0 Comments