Header Ads Widget

FAINALI YA ANNE KILANGO CUP KUTIMUA VUMBI KESHO..

 


NA WILLIUM PAUL, SAME 

HAYAWI hayawi sasa yamekuwa nani kubeba mwali katika fainali za michuano ya mpira wa miguu ya kombe la Anne Kilango cup hiyo kesho.


Ni mashindano ya aina yake ambayo hayajapata kutokea ya Anne Kilango cup yanayofadhiliwa na Mbunge wa Jimbo la Same mashariki, Anne Kilango Malecela.



Kivumbi cha fainali kinachotarajiwa kutimua vumbi kesho katika uwanja wa Miamba ambapo utawakutanisha miamba miwili ya soka timu ya Kirangare kutoka kata ya Kirangare na timu ya Mpinji kutoka kata ya Mpinji.


Mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 20 kutoka katika Tarafa ya Miamba ambapo Kirangare iliingia fainali baada ya kuifunga timu ya Vunta goli mbili kwa moja huku Mpinji ikiifurumusha Miamba kwa jumla ya goli tatu kwa mbili.



Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Same mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye ndio mdhamini wa mashindano hayo alisema kuwa mbali na kombe mshindi ataondoka na zawadi nono pamoja na mshindi wa pili na watu huku timu zote 20 zilizoshiriki michuano hiyo zinatarajiwa kuondoka na zawadi.


Anne Kilango alisema kuwa, mgeni rasmi katika fainali hiyo atakuwa Mkuu wa wilaya ya Same, Edward Mpogolo.

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI