Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi Joseph Roman Selasini amesema kuwa msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Fransis Mutungi ameridhia vikao vyote vilivyofanywa na chama hicho pamoja na Mkutano Mkuu kuwa ni halali hivyo mabadiliko ya viongozi yaliofanywa na Mkutano Mkuu ni halali kwa mujibu wa sheria.
Kauli hiyo, ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kwa sasa viongozi waliochaguliwa na Mkutano Mkuu ni viongozi halali wa chama hicho hivyo endapo akitokea mtu kulitumia jina la Chama hicho atachukuliwa hatua.
"Kulikuwa kuna mkanganyiko wa makundi mawili kila moja lilikua linataka kuongoza lakini sasa Mkutano Mkuu umeshatoa majibu ya maswali yote, sisi ndio wenye mamlaka na sio hao wanaotumia jina la Chama vibaya"amesema Selasini.
Aidha, amemuomba IGP Camilius Wambura kuyafanyia kazi mashauri yote yaliyopo mezani kwake, na kuwachukulia hatua wote wanaotumia jina na vyeo vya chama hicho kwani wanatenda kinyume na Sheria ya chama hicho.
Hata hivyo, amesema hawatomvumilia mtu yoyote atakae tumia jina hilo vibaya ama kuandika vyeo ambavyo wanaotumia sio viongozi basi hawatosita kumchukulia hatua za kisheria.






0 Comments