Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Ile siku ambayo ilikua ikisubiriwa kwa hamu ya kumpata mshindi wa mister na miss kiziwi wa dunia inahitimishwa kesho katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa (JNICC) kuanzia majira ya saa tisa alasiri ambapo washriki kutoka nchi 47 duniani watachuana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es SalaamKatibu Mkuu wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas amesema mgeni rasmi anatarijiwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu, Dorothy Gwajima ambapo majaji kutoka nchi mbalimbali tayari wameshawasili nchini Tanzania huku washiriki 400 wanatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo.
Aidha amewasihi washiriki wa mashindano hayo kutambua kuwa kuna kushindwa na kushinda hivyo wawe wastaarabu kupokea matokeo yoyote kutoka kwa majaji, kwani hadi kufikia hatua ya kupeperusha bendera za nchi zao kufikaTanzania kushiriki tayari wamefanya mambo makubwa katika ushiriki wao.
Amesema kuwa, washindi wa shindano hilo watapata fursa yakutembelea hifadhi ya ngorongoro na kufanya Utalii ambapo hatua hiyo ni sehemu yakuitangaza Tanzaia katika sekta ya Utalii.
'" Tumepewa heshima kubwa, na sisi kama Serikali tumelichukulia kwa uzito suala hili, tunatarajia wageni elfu moja mia nne watahudhuria,hivyo nawaomba wale wote walioalikwa wajitokeze kwa wingi ili kufanikisha mashindano haya" amesema Dkt Abasi
Kwa upande wake, Rais wa Dunia wa Viziwi, Bonita Annleek amesema kuwa Serikali ya Tanzani imefanya maandalizi mazuri ya mashindano hayo ambapo pia amesisitiza kuwa wataendea kuwa na mahusiano mazuri kati ya nchi ya Tanzania na nchi zingine.
"Nimefurahi sana kuona Tanzania inajali kundi hili la viziwi, kwakuwekeza fedha kuweza kufanikisha mashindano haya yakidunia, Oktoba 31.2022 washindi wamepata fursa yakwenda kutembelea Hifadhi ya ngorongoro mara baada ya mashindano haya kumalizika hivyo fursa hii ni muhimu kwao na waitumie" amesema Bonita.
Nae, Raisi wa Viziwi Afrika, Habibu Mlope amesema kwamba awamu hii ni mara ya pili Tanzania kushiriki mashindano ya Mister and Miss Kiziwi hivyo haina budi kuishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kwa utendaji wake uliotukuka.
Nao baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wamebainisha kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha n akwamba wapo tayari kupanda jukwaani na kushiriki Mashindano hayo.
Aidha katika siku hiyo kutakuwa na burudani za za kutosha kwani Z Antoni na Mziki wake wa nimpate wapi Binti Kiziwi uliosheheni kisa chake atakuepo na Sholo Mwamba na Taarabu ya Pwani wote kwa pamoja waliyapamba mashindano hayo.









0 Comments