MWENYEKITI wa URA Saccos, Benedict Wakulyamba amesema wamefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya sh Bilioni 394.5 sawa na asilimia 75 ambazo zilitumika katika ujenzi wa nyumba, huku huduma nyingine za mtu mmoja mmoja zikitolewa kwa wanachama wagonjwa, huduma ya vifo kwa wanachama na wategemezi wao, fidia kwa majanga dhidi ya wanachama.
Amesema saccos hiyo ilianza mwaka 2006 ikiwa na wanachama 4300 huku wakati huo ikiwa na hisa ya sh 17,026,693 na sasa wana hisa ya sh 8,421,327,680 na wanachama 46,024 kutoka pande zote za nchi.
Wakulyamba amesema mwaka 2021 walitoa gawio la fedha taslimu sh 1,082,539,598 na walitoa akiba ya sh 3,357,065,139 waliwezesha sh 415,000,000 kwa hospitali, zahanati na vituo vya afya zinazomilikiwa na polisi nchini.
Pia aliipongeza serikali kwa kuimalisha mifumo na kusimamia, kuongeza mishahara na kupandisha vyeo kwa watumishi wa umma.
Amesema mikopo iliyotolewa ni juhudi za serikali za kuboresha maslahi ya watumishi wa umma.
Naye Mrajis Msaidizi wa Vyama vya fedha kutoka tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Josephat Kisamalale amewapongeza polisi kwa kujiunga na saccos hiyo na kupelekea kuwa na wanachama wengi tofauti na saccos nyingine nchini.
Amesema kuna umuhimu wa kuanzishwa kwa Saccos kwani inasaidia serikali katika utoaji wa fedha kwa jamii.










0 Comments