Header Ads Widget

PROF. NDALICHAKO MGENI RASMI TUZO ZA VIJANA CHIPUKIZI ZA TEYA-AGOSTI 27

 


Na Andrew Chale,


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tuzo za Vijana chipukizi za TEYA zitakazofanyika Agosti 27, ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.


Wakizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam jana , Agosti 17, Waratibu wa tuzo hizo pamoja na Wadau wake  wamebainisha kuwa tuzo hizo za Vijana Chipukizi Tanzania zinatoa ari na kuhamasisha vijana kupanua fikra inayowawezesha kuwakomboa kiuchumi kwa kutangaza shughuli wanazozifanya kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( Tehama).


Mjumbe wa Bodi wa Shirika la Africa Youth Transformation, Paul Siniga  alisema AYT imeandaa tuzo hizo kwa kuamini itabadilisha mtazamo wa fikra kwa vijana kwa kuwa imeonekana  wakipewa majukumu mbalimbali wasimamie wanaweza.


Alisema Shirika limekuwa likishirikisha vijana katika kampeni mbalimbali ikiwemo  ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwaelimisha wayatunze mazingira.


"Pia tunatoa elimu ya afya na uzazi ili vijana wajiepushe na majanga mbalimbali yanayoweza kuwakumba," alisema.



Kwa upande wake, Ofisa kutoka Shirika hilo, Saraphina Lelo alisema sehemu nyingi ya vijana wamekuwa sio wanufaika wa maendeleo bali watazamaji wa program na sera zinazoathiri maendeleo yao.


Alisema kupitia tuzo hizo ambazo ni sehemu ya usaidizi wa utekelezaji wa sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 zinalenga kuwafikia vijana wote walioonyesha mchango chanya katika sekta mbalimbali za kimaendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.


"Kwa mwaka huu wa 2022, Tuzo za Vijana chipukizi inategemea kutoa tuzo katika kipengele 40 ambapo vijana walishindana na siku rasmi ya kilele cha sherehe itakuwa kwa siku tatu na itaanzia Agosti 25, 26 na 27 Agosti mwaka huu," alisema.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Habari kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA), Semu Mwakyanjala alisema zaidi ya nusu ya watanzania ni vijana maana yake ni kwamba Ndio tegemeo kubwa la nchi.


Alisema wameunga mkono jitihada hizo kwa kuwa moja ya jukumu walilonalo ni kukuza Teknolojia ya Habari na Mawailiano ( Tehama) ambapo ndilo eneo wanalolipenda vijana.


Naye Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Haki na Mtoto Save International, Besta Mulauzi alisema wanafanya shughuli zao kwa zaidi ya nchi 100 duniani ambazo zimelenga kwenye afya, elimu, haki za watoto na maeneo mengine.


Alisema huu ni mwaka wa pili wanafadhili tuzo hizo.


Kwa mwaka huu wa 2022, Tuzo za vijana chipukizi (TEYA) inategemea kutoa tuzo katika vipengele 40 


Aidha, walisema kuwa, Tiketi zitakuwa za aina tatu ambazo ni; 


"Tiketi ya 15,000 ambayo ni daraja la kawaida.

Tiketi ya 50,000 ambayo ni daraja la biashara.

Tiketi ya 100,000 ambayo ni daraja la juu (VIP)

Kwa siku ya tatu yaani Agosti 27, 2022, 



Aidha, kamati ya maandalizi ya Tuzo hizo za vijana chipukizi (TEYA) kwa niaba ya taasisi yaani Africa Youth Transformation (AYT) imetoa shukrani  za dhati kwa ushirikiano kutoka kwa Serikali, wadau wa maendeleo mbalimbali kwa makundi yao na vyombo vya habari katika kuhakikisha dhima na lengo kuu la tuzo hizo linafikiwa. 




AYT  ni shirika linaloongozwa na vijana, lisiloegemea upande wowote, lisilo la faida, lisilo la kiserikali [NGO] lililoanzishwa mwaka wa 2018 na lilisajiliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Julai 19, 2019, yenye nambari ya usajili [00NGO/R/0180] kufanya kazi kama Asasi Zisizo za Kiserikali; inayolenga kukuza haki za kiuchumi na kijamii, amani, pamoja na kuboresha upatikanaji rafiki wa vijana katika elimu, afya na ushirikishwaji wa jamii ili kuondokana na umaskini nchini Tanzania.


Tuzo hizo ni kulingana na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana Tanzania (2007) inamuelezea kijana kama Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 35. Pia, kulingana na Sensa ya 2012, vijana ni asilimia 53.8% ya idadi yote ya watanzania. 



Ambapo tayari vijana hao mbali mbali wanapigiwa kura mtandaoni kupitia mitandao n tovuti ya tuzo hizo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI