Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,ameagiza kukamatwa kwa mkandarasi ambae alikuwa akitekeleza mradai wa soko la samaki wabichi katika mwalo wa Chifunfu mkoani Mwanza baada ya mradi huo kutokamilika kwa wakati na akiwa tayari amelipwa zaidi ya sh. milioni 90 ambapo ghalama ya mradi ni shilingi milioni 120
" Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega,amesema serikali aitakubali kuona wakandarasi wanakula pesa za kutekeleza miradi ya wananchi hivyo wizara itamchukulia hatua mkandarasi ambae alikuwa akitekeleza ujenzi wa soko la samaki wabichi katika mwalo wa Chifunfu wilayani Sengerema mkoani Mwanza,kwa kutoa ripoti bodi ya wakandarasi ili aweze kufungiwa na kuondolewa katika orodha ya wakandarasi nchini
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega,ameagiza Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini ( TAKUKURU ) wilayani Sengerema mkoani Mwanza,kumchukulia hatua mkandarasi ambae anatekeleza mradi wa ujenzi wa soko la samaki wabichi katika mwalo wa chifunfu baada ya kuchukua muda mrefu katika utekelezaji wake
" Mbunge wa Jimbo la Sengerema Tabasam Hamis,ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kumchukulia hatua mkandarasi wa ujenzi wa soko la samaki katika mwalo wa Chifunfu uliopo wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza baada ya kuchelewa kutekeleza ujenzi kwa wakati na serikali ikiwa imelipa zaidi ya sh,milioni 90 kwa ajili ya mradi huo.
0 Comments